Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe akiwahutubia wananchi wa kijijicha Tumaini leo wakati akihamasisha michenzo ndani jimbo hilo. |
Na George Mwigulu,Nsimbo.
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe amedhamiria kuwaunganisha wasanii wa mziki wa kizazi kipya na muziki wa ngoma asili wa Jimbo hilo kwenye mfuko wa taifa wa utamaduni ili waweze kunufaika na mikopo ya fedha itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.
Amesema hayo leo wakati wa hafla ya bonaza la kuibua vipaji vya Sanaa ya musiki katika kijiji cha Tumaini Kata ya Itenka Halmashauri ya Nsimbo mkoa hapa ambapo ameeleza nia yake ya kukuza sio mchezo wa mpira wa miguu pakee bali hata michezo mingine hususani pia sanaa.
Lupembe
amesema kuwa kupitia bonaza hilo ameona vipaji mbalimbali jinsi ambavyo vijana
wanaiba na kucheza jambo ambalo limemvutia sana na kuona namna bora ya kuwasapoti
waweze kukua zaidi kwenye sanaa hiyo.
‘’… tumechenza ngoma na tumeona vipaji vya kwaya mbalimbali hapa,Ndugu zangu vikundi vyote vya ngoma mliojiandikisha mlioimba hapa ninawaingiza kwenye kundi la mfuko wa utamaduni wa taifa tutakuja kufanya uwasajili na BASATA itakuja kuwasajili na kuanza kupewa mikopo’’ amesema Lupembe.
Mbunge huyo ametoa rai ya kuacha tabia ya baadhi ya vikundi vya ngoma kuanzishwa na kupotea,Hivyo kuvitaka vikundi vyenye tabia hiyo kuacha sambamba na kutokujiandikisha kwa sababu fedha za mkopo watakazopewa lengo lake ni kunufaisha kundi,jamii ya Itenka na taifa vilevile mrejesho utatolewa kwa mfuko wa utamaduni wa taifa.Aidha
kwa mwaka huu ameweza kuhamasisha Sanaa ya utamaduni maarufu kama ‘‘mbina’’ au ‘’
matanda’’ ambayo yatafanyika mwenzi wa tisa na kujumuisha makundi ya Sanaa ya
jimbo lote la Nsimbo.
Aidha katika bonaza hilo mbunge huyo ameweza kutoa fedha Jumla Tshs 2,340,000/= kama zaidi kwa washindi wa vikundi vya ngoma za asili ,kwaya na waibaji binafsi wa mziki wa kizazi kipya ambapo mshindi wa kwanza amepewa fedha Tshs 300,000/-,Mshindi wa Pili Tshs200,000/- watatu Tshs 100,000/-na wa mwisho Tshs 50,000/- kwa kila makundi husika shindaniwa.
Naye kiongozi wa kundi la ngoma asili Sumu ya Mamba,Maria Nyango amemshukuru mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe kwa kuweza kuona kuwa Sanaa ya uimbaji inanafasi ya kuwakomboa kiuchumi.Ameeleza
kuwa Sanaa ni ajira ambayo kama itathaminiwa na wadau mbalimbali itaweza kukua
zaidi katika Mkoa wa Katavi.
Vilevile
Zengo Tuma,Mkazi wa kijiji cha Itenka A amesema kuwa kuingizwa kwenye mfuko wa
taifa wa utamaduni sio tuutawawezesha wasanii kupata mikopo ya kifedha bali ni
lango la wasanii kutambulika kitaifa.
Hivyo
akawaasa wasanii wa jimbo Nsimbo kuchangamkia fursa hiyo kwa kuhakikisha
wanafanya kazi nyingi za Sanaa huku wakindumisha umoja na mshikamo.
Tizama hapa chini moja ya ngoma ya Sumu ya Mamba wakicheza.