MBUNGE LUPEMBE WANAMICHEZO JENGENI UPENDO KUFIKIA MAFANIKIO.

 

Anna Lupembe(wa kwanza kushoto),Mbunge wa Jimbo la Nsimbo akitoa fedha kwa baadhi ya washindi katika bonaza na miziki ambapo limefanyika leo katika Kata ya Uruwila.

Na George Mwigulu,Nsimbo

Wanamichezo hususani wa mpira wa miguu wametakiwa kujenga umoja,mshikamano na upendo miongoni mwao wakati na baada ya kumaliza kushiriki michezo katika ligi ya Lupembe Cup.

Baadhi ya wanashi wakipewa zawadi ya fedha na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe(wa kwanza kushoto)

Wanamichezo hususani wa mpira wa miguu wametakiwa kujenga umoja,mshikamano na upendo miongoni mwao wakati na baada ya kumaliza kushiriki michezo katika ligi ya Lupembe Cup.

Amesema hayo leo Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe katika kata ya Uruwila wakati akishiriki bonaza la muziki wa ngoma za asili,kwaya na muziki wa kizazi kipya.

Bonaza hilo ambalo limelenga kuibua vipaji vya wanamuziki mbalimbali sambamba na kuwasajili ili kuwaingiza kwenye mfumo wa mfuko wa taifa wa utamaduni ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo ya fedha.

Baadhi ya vikundi mbalimbali vikitubuhiza kwenye bonaza la ngoma asili,kwaya na muziki wa kizazi kipya  katika kata ya Uruwila Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi.


Lupembe amesikitishwa kutokana na baadhi ya vijana kuwa chanzo cha vurugu na kupigana wakati wa michenzo jambo ambalo linatishia hali ya usalama wa wachezaji wa mpira wa miguu na wapenzi wa mchenzo huo.

Amesema kuwa ameleta mashindano ya mpira wa miguu ili kuibua vipaji vya vijana na kuwaunganisha kuwa ndugu kwa kuwa michenzo ni furaha,ajira,Amani na upendo.

Amesema mbunge huyo “ katika kata ya Uruwila michenzo imekuwa uwadui na sio michezo furaha na Amani…tambue michezo iko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi  na mimi kama mbunge ndio maana nafanya hivi kutokana na ilani ya CCM inanielekeza lakini hapa mpira haukuchezeka,fujo kupigana hadi kuumizana na kuwa jambo la hatari”.

Mbunge huyo amesisitiza kuwa ili wachezaji waweze kufikia ndoto za kuwa wachezaji wakubwa kama vile Samatta na Mayele suala la nidhamu kwenye mchezo wanapaswa kulizingatia ili kuonesha vipaji pekee na sio vurugu.

Aidha katika hatua nyingine Mbunge huyo ameweza kutoa fedha kama zawadi kwa washindi mbalimbali wa ngoma za asili,muziki wa kizazi kipya na kwaya.

Ambapo kwenye kila kundi la washindi wanne wa ngoma za asili,muziki wa kizazi kipya na kwaya,Mshindi wa kwanza amepewa fedha Tsh 300,000/-,wa pili Tsh 200,000/- wa tatu Tsh 100,000/-na mshindi wan ne Tsh 50,000/- ikiwa mshindi wa kwanza na wapili moja kwa moja wataingia kwenye mashinda ya ngazi ya jimbo yatakayofanyika mwezi wa tisa mwaka huu.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages