Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki akizungumza na wanawake wa UWT kata ya Machimboni ambapo amewaasa kusaimama imala katika malezi ya watoto wao. |
Na Paul Mathias,Nsimbo
Baadhi ya Wazazi na walezi Katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wameonywa kutowatumikisha watoto katika Shuguli za uchimbaji wa Madini na badala yake wahakikishe watoto wao wanawapeleka Shule ili wapate Elimu.
Muonekano wa Shuhguli za uchimbaji wa Madini katika Kata ya Machimboni ambapo baadhi ya wazazi huwatukisha watoto katika kazi hizo |
Baadhi ya Wazazi na walezi Katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wameonywa kutowatumikisha watoto katika Shuguli za uchimbaji wa Madini na badala yake wahakikishe watoto wao wanawapeleka Shule ili wapate Elimu.
Wito
huo umetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki wakati wa
ziara yake ya kutembelea Kata za Mkoa wa Katavi alipokuwa anazungumza na Umoja
wa wanawake UWT kata ya Machimboni pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi.
Amesema
kuna tatizo la baadhi ya wazazi kuwatumikisha watoto wadogo katika shughuli za
uchimbaji wa Madini kwa ujira mdogo kitu ambacho ni kinyume na sheria hali
ambayo huwafanya baadhi ya watoto kuacha shule au kuwa watoro kwa kujiingiza
katika kazi hizo.
Mbunge wa Viti maalumu Martha Mariki [Kulia] akisalimiana na Vikundi vya Ngoma ya Asili apofika katika Kata ya Stalike. |
Mbunge huyo anasema ‘’ajira kwa watoto hairuhusiwi watoto hawa wanatakiwa waende Shuleni mfano wewe unamgodi wako unawatumikisha watoto katika eneo lako la Machimbo hiloharikubariki sheria inasema nikosa kwa mtoto kumwajili chini ya miaka 18 nilazima achukuliwe hatua kwani anamnyima haki ya kupata masomo ‘’amesema Mb Martha
Ameeleza
kuwa kazi ya Machimbo huhitaji watu wenye umri mkubwa ambao wapo juu ya miaka
18 hivyo kuwa fanyisha kazi hizo nzito machimboni niku hatarisha usalama wao
kwani hufanya kazi ambazo haziendani na umri wao.
‘’kwanza
unamfanyisha kazi mtoto huyu ambazo si za umri wake sheria zinasema ili mtu
aweze kufanya kazi lazima afikishe miaka 18 ili aweze kujitambua na kuingia
mkataba wa kazi husika anayoifanya tatizo hili niliambiwa pia katika Kata ya
Magamba wazazi tuwajibike katika hili ‘’amesisitiza Mb Martha
Diwani wa Kata ya Stalike Adam Chalamila[kushoto]akiteta jambo na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki akiwa katika Kata ya Stalike |
Katika hatua nyingine ameziomba Jumuiya za Wazazi na UWT ngazi ya Kata kuhakikisha wanatembelea Shule ili kujiridhisha mwenendo wa Mahudhurio ya Wanafunzi shule ili iwe rahisi kuchukua hatua kwa wazazi ambao watabainika kuwatumia watoto hao katika shughuli za uchimbaji wa Madini.
‘’jumuiya
ya wazazi mpo hapa jumuiya ya wanawake mpo hapa nendeni shuleni mkafatilie
mienendo ya watoto Shuleni huko wapi ni Watoro wapi ambao hawaendi shuleni wamekimbilia
Shughuli za Machimbo’’ameeleza Mbunge huyo.
Awali
akiwa katika Kata ya Stalike ameishukuru serikali kwa kuendelea kudumisha
huduma za jamii katika Nyanja ya Elimu,Afya,Barabara na Maji kwa mkoa wa Katavi
na katika Kata hiyo kwa lengo la kusogeza Huduma Karibu na wananchi.