WANAWAKE UWT WAHAMASISHWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki akiwahutubia wananchi katika Kijiji cha Mchangani katika Kata ya Ikola.

Na Paul Mathias,Tanganyika

Wanawake wa Umoja wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tanganyika Mkoa Mkoa wa Katavi wameobwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uchaguzi wa Serikali za mitaa utakao fanyika mwaka kesho .

Wanawake wa Umoja wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tanganyika Mkoa Mkoa wa Katavi wameobwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uchaguzi wa Serikali za mitaa utakao fanyika mwaka kesho .

Akizungumza na wananchi Katika Kata ya Isengule na Kata Ikola katika ziara yake ya kutembelea kata Kwa Kata Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki amesema wanawake  wasiogope kuingia katika mchakato wa uchaguzi ngazi za Serikali za mitaa utakao fanyika mwakani.

''niwaombe akina mama wenzangu katika Kata hii ya Isengule na Ikola tusiogope kuingia kuwania nafasi hizo sisi wanawake ni jeshi kubwa ''amesema Mariki.

Amesema Chama Cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya UWT kina amini jumuiya Hiyo inamchango mkubwa katika ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi Mbalimbali 

Katika hatua nyinginee amewasa akina mama na Jamii Kwa ujumla kuzingatia malezi ya watoto Kutokana na changamoto ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili wa kijinsia 

"Sasa hivi ndungu zangu Kuna shida ya tatizo la ulawiti Kwa watoto wa kiume na ukatili Kwa watoto wa kike hali hii tuipinge Kwa nguvu ukiona kunaviashiria ya vitendo hivyo toa taarifa Kwa viongozi Kwenye eneo lako"

Amesema kuwa tatizo Hilo la unyanyasaji wa wa kijinsia limekuwa likibeba sura nyingi ikiwemo Imani potofu Kwa baadhi ya jamiii.

Mbunge huyo akiwa katika kata za Ikola na Isengule ameweza kutoa shilingi laki Tano Kwa kila kata Kwa lengo la kuwasaidia wanawake wa UWT kujikwamua kiuchumi Kupitia vikundi vya kiuchumi.

Ziara hiyo inaendelea katika kata za Kasekese na Kata ya Sibwesa zilizopo Wilaya ya Tanganyika Kwa lengo la kuongea na wanahama na wanawake wa Jumuiya ya UWT pamoja na kuwaelezea utekelezaji wa miradi ya Maendeleo inayoletwa na serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk samia Suluhu Hassani.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages