Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki akizungumnza na wanawake wa UWT Katika Kijiji cha Kajeje Kata ya Kanoge. |
Na Paul Mathia,Nsimbo
Mbunge wa Viti
maalumu mkoa wa Katavi ,Martha Mariki amekabidhi hundi ya Shilingi Milioni Tano
kwaajili ya kusaidia ukarabati wa Jengo la mama na Mtoto katika Kijiji Cha Kajeje iliyopo Kata ya Kanoge Halmashauri ya
Nsimbo Mkoa wa Katavi.
Mbunge wa Viti Maalumu Martha Mariki [alieshika Maiki] akiwa katika picha na viongozi wa Kata ya Kanoge na uongozi wa Kijiji cha Kajeje akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni Tano |
Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi, Martha Mariki amekabidhi hundi ya Shilingi Milioni Tano kwaajili ya kusaidia ukarabati wa Jengo la Mama na Mtoto Katika Kijiji Cha Kajeje Kata ya Kanoge Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi.
Akiwa katika kikao
katika Kijiji cha Kajeje Mbunge Martha Mariki amesema kwa kutambua Juhudi
zinazofanywa na serikali katika kuimalisha miundombinu ya Afya katika Mkoa wa
Katavi na Halmashauri ya Nsimbo kwa
ujumla na kuchangia Milioni Tano ili kuharakisha ukarabati Jengo la Mama na Mtoto.
‘’ndugu
zangu wana Kajeje Mimi Mbunge wenu wa Mkoa wa Katavi nimeguswa na Risala yenu
nawachangia Milioni Tano ili kusaidia ukarabati huu wa Jengo la mama na Mtoto ili
wanawake wenzangu wapate huduma bora wakija kujifungua hapa’’amesema Mbunge
Martha.
zahanati ya Kijiji cha Kajeje ambayo Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki ametoa shilingi Milioni Tano ili kusaidia ukarabati wa Jengo la Mama na Mtoto. |
Ameeleza kuwa miongoni mwa Mambo ambayo serikali imekuwa ikiyafanya katika mkoa wa Katavi nikuendelea kujenga Zahanati,Vituo vya Afya ,Hospitali za Wilaya pamoja na uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambayo imeanza kufanya kazi na kuwaepushia adha wananchi kwenda kutibiwa katika Mikoa mingine.
‘’Niwaambie
ndungu zangu mkoa wetu unahalmashauri Tano Tayari serikali imesha Jenga Vituo
vya afya,na kujengwa kwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi Eneo la Kazima hii
ni hatua kubwa ya mapinduzi ya utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wetu
tunaishukuru sana serikali kwa hili’’amesema Mbunge Martha Mariki.
Salehe Mrisho Diwani
wa Kata ya Kanoge amemshukuru Mbunge huyo kwakuwaonea Huruma akina mama wa
Kijiji cha Kajeje kwa Kuguswa na kuchangia Milioni Tano katika ukarabati wa Jengo la mama na Mtoto..
Wananchi wa Kijiji cha Kajeje wakimsikiliza Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki |
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Nsimbo Charles Halawa amesema kuwa wanamshukuru sana Mbunge
Martha Mariki na kwa Mchango wake na wao kama halmshauri tayari wametenga
Milioni Hamsini kwaaajili ya ukarabati wa wa Jengo hilo la mama na Mtoto katika Kijiji cha Kajeje
‘’Mh Mbunge kazi uliyoifanya ya kutoa milioni Tano ni kazi kubwa sana katika jengo hili la mama na Mtoto niukweli usiopingika kijiji hiki cha Kajeje wananchi wamekuwa wakipata adha katika eneo hili la afya lakini naamini sasa kutoa kwa hiii Milioni Tano itasaidia ukarabati huu’Amesema mwenyekiti Halawa
Ziara ya ya Mbunge Viti maalumu katika Mkoa wa Katavi Martha Mariki inaendelea ka Katika Wilaya ya Mpanda Hususani Jimbo la Nsimbo ambapo ametembea Kata ya Kanoge na Katumba na kutoa shilingi laki Tano kwa kila kata kama sehemu ya kuimarisha Jumuiya ya UWT Kwenye Kata hizo pamoja na kutoa Kadi za UWT ili jumuiya hiyo iendelee kuingiza wanachama wengi zaidi wa UWT.