MBUNGE MARTHA MRADI WA BOOST UTABORESHA SEKTA ELIMU TANGANYIKA.


Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki alipotembelea mradi wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule ya Msingi kasekese unaotokana na fedha za Mradi wa Boost.

Paul Mathias na George Mwigulu,Katavi.

Mbunge wa viti maalumu kupitia chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Martha Mariki amesema uwekezaji unaofanywa na Serikali Katika sekta ya Elimu kwenye eneo la miundombinu Katika Wilaya ya Tanganyika unatija Katika kutatua changamoto ya miundombinu ya Elimu.

Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki akipitia taarifa ya ujenzi wa Madarasa katika shule ya Msingi kasekese yanayo jengwa kwa Fedha za Boost.

Mbunge wa viti maalumu kupitia chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Martha Mariki amesema uwekezaji unaofanywa na Serikali Katika sekta ya Elimu kwenye eneo la miundombinu Katika Wilaya ya Tanganyika unatija Katika kutatua changamoto ya miundombinu ya Elimu.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea Kata zote za mkoa wa katavi,Akiwa Katika Kata ya Kaseseke ambapo ameweza kutembelea shule ya Msingi Kaseseke na kujionea ujenzi wavyumba vya Madarasa kupitia Mradi wa Boost.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi Martha Mariki akipata maelezo ya utoaji huduma ya afya katika kituo cha afya Sibwesa .

"tunaishuru Serikali yetu Kwa kuja na mpango huuu wa Boost tumeona ujenzi ukiwa unaendelea  hii inaonyesha adhima nzuri  ya kuendelea kuboresha Miundo mbinu ya Madarasa kwenye shule za msingi kwenye wilaya na Tanganyika '' Amesema Martha.

Amewaomba wananchi hususani wakazi wa Kaseseke kuendelea kuwekeza katika Elimu kwa kusomesha watoto wao kwakuwa Serikali imeendelea kuwekeza katika Elimu.

Katika ziara hiyo ameweza kutembelea Kituo Cha Afya Sibwesa ambapo ameipongeza Serikali Kwa kuona umuhimu wa kujenga kituo Cha Afya Sibwesa ili wananchi waendelee kupata huduma za Afya kwenye karibu na makazi yao.

Ameeleza Mbunge huyo "Hongereni Sana wanasibwesa Kwa kujengewa kituo Cha Afya hii inaonyesha dhamira ya Serikali kusogeza huduma karibu Kwa wananchi kitumieni kituo hiki Cha Afya vizuri Serikali imejenga kwaajili yenu".

Katika hatua nyingine ameipongeza halmashauri ya Tanganyika Kwa kuanza ujenzi wa jengo la akina mama katika kituo hicho na kuiomba halmashauri hiyo kuongeza Kasi katika ujenzi huo ambao unatekelezwa kupitia Mapato yake ya ndani.

"naipongeza halmashauri Kwa kuona umuhimu wa kuanza ujenzi wa jengo hili la akina mama katika kituo hiki kupitia Mapato ya ndani niwaombe kuongeza nguvu katika ujenzi huu ili jengo hili likamilike Kwa wakati"

Mbunge huyo amezungmza  na Viongozi wa Umoja wa Jumuiya ya wanawake wa UWT Kata za Sibwesa na Kaseseke na kutoa shilingi Laki Tano Kwa Kila Kata kwaajili ya kuwainua kiuchumi pamoja na kutoa kadi 2000 za UWT Katika mkoa wa Katavi na Kutoa Jalala 120 kwa UWT .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages