Na Walter Mguluchuma,Katavi.
Serikali chini ya Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kupitia mradi wa Tanzania ya Kidigitali inatarajia kujenga minara ya mawasiliano katika Mkoa wa Katavi ili kuimarisha mawasiliano kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani humo.
Hayo amesema leo Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhadisi Kundo Mathew katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi akiwa kwenye ziara ya kikazi ambapo alisema kuwa maeneo ambayo itajengwa minara hiyo ni katika kata za Kasasa,Majimoto,Bulamata,Ipwaga,Kasekese,Katumba na Uruwila.
Mhadisi Kundo ameeleza kuwa kujenga mnara wa
mawasiliano moja gharama yake ni wastani wa fedha Mil 350 ikiwa ni sawa na ujenzi wa kituo
kimoja cha afya lakini serikali imeamua kuwekeza fedha zote hizo kwenye kujenga
minara kwa sababu inatija.
Amesema kuwa tija inayopatikana kupitia mawasiliano
ni pamoja na wananchi wataweza kuwasiliana na
vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa za kiharifu
Vilevile mawasiliano ni afya kwani mtu anapopata
changamoto yoyote ya kiafya anauwezo wa kuita gari la wagonjwa sambamba na
kurahisisha taarifa kwa jeshi la zimamoto pale majanga ya moto yanapojitokeza.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa katika kuhakikisha
Tanzania inakuwa chini ya uchumi wa kidigitali (Digital Economy) serikali
ilianzisha sheria namba 11 ya mwaka 2006 ya mfuko wa mawasiliano kwa wote.
Mfuko wa mawasiliano kwa wote lengo lake ni kutoa fedha za ruzuku kwa makapuni ya mitandao ya simu pale ambapo wakiona kama wakiwekeza watapata hasara kwa kukosa faida basi serikali itasaidia ili wasipate hasara na huduma ya mawasiliano kupatikana kwa wananchi wote.
“…mwenzi uliopita kunautiaji saini wa mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano katika nchi nzima ambapo minara 758 inaenda kujengwa ambapo serikali inakwenda kutoa fedha za ruzuku Bilioni 126 ni sawa na asilimia 40 inakwenda kujenga minara hiyo “ Alisema Kundo.Ameeleza lengo ni kuhakikisha maeneo yote ambayo
hayana mvuto wa kibiashara,maporini yenye uhitaji wa mawasiliano na maeneo ya
pakani serikali itahakikisha wananchi wanawasiliano kupitia mitandao husika ya
nchini ili kuepuka kutumia mitandao ya nchi jirani.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Onesmo Buswelu amemwomba Naibu Waziri huyo uharakishwaji wa ujenzi minara ya mitandao ya simu mkoni humo kwani wamezindua huduma ya M-Mama kwa lengo la kusaidia wanawake wajawazito wanaopata changamoto pindi ya kujifungua kwa kukosa mtandao ya simu pindi wanapotaka kutoa taarifa kwa gari la wagonjwa.
Buswelu amesema kuwa huduma ya M-Mama itakuwa na ufanisi mkubwa kwani hakuna atakaye kosa huduma ya afya kutokana na changamoto ya mtandao wa simu.Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,Jamila Yusuph amesema kuwa
maisha kwa sasa yanategemea sana mawasiliano ya kimtandao kutokana na kuwa hurahisisha
namna ya kutoa na kupokea taarifa za kijami.
Aidha ameishukuru serikali kwa mpango wake wa
ujenzi wa minara ambayo itakwenda kuimarisha zaidi usalama wa watu kutokana na
jiografia ya mkoa huo kuwa mpakani nan chi jirani.