MIKOPO YA ASILIMIA KUMI MKOMBOZI WA UCHUMI KWA VIJANA NA WANAWAKE

 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki [Katikati] akiwa katika kikao na Wanawake wa UWT kata ya Shanwe

Na Paul Mathias,Katavi 

Wanawake, vijana na watu wenye uleamavu Katika mkoa wa Katavi wameaswa kuchangamkia fursa ya Mikopo ya Asilimia Kumi ambayo imekuwa ikitolewa na halmashauri ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kufanya Shughuli mbalimbali za kiuchumi .

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki [wa Pili Kulia ]akiwa kabidhi shilingi laki Tano Wanawake wa UWT kata ya Shanwe Huku diwani wa Kata hiyo Hafidhi Masumbuko[Katikati] akishuhudia utolewaji wa Fedha hiyo

Wanawake, vijana na watu wenye uleamavu Katika mkoa wa Katavi wameaswa kuchangamkia fursa ya Mikopo ya Asilimia Kumi ambayo imekuwa ikitolewa na halmashauri ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kufanya Shughuli mbalimbali za kiuchumi .

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi wakati akizungumza na wanawake wa UWT Katika Kata ya Shanwe na Kasokola zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi katika ziara anayoendelea nayo ya kutembelea Kata 58 za Mkoa wa Katavi.

Mbunge huyo amesema kuwa serikali imeanzisha Mfumo huo wa Kutoa fedha za Mikopo kwa Makundi ya Vijana,Wanawake, na Walemavu kwa la kuhakikisha Makundi hayo yanajikwamua kiuchumi.

‘’Mikopo hii imekuwa ikitolewa kwa akina mama Asilimia Nne Vijana Asilimia Nne na watu wenye Mahitaji Maalumu Asilimia Mbili niwaombe sana tuendelee kutumia fursa hii najua kwa sasa serikali inajipanga ni namna gani iendelee kutoa mikopo hii niwaombe sana mchangamkie Fursa hii inayotolewa na serikali yetu’’

Ameeleza kuwa baadhi ya wanufaika wa Mikopo hiyo tangu ianze kutolewa na serikali imewanufaisha kwa kiwango kukubwa kwa kubadilisha maisha yao ya kiuchumi kupitia Miradi wanayoifanya kupitia fedha hizo za Mikopo ya halmashauri.

Katika kuhakikisha uchumi wa UWT katika kata hizo unaimalika Mbunge huyo ametoa shilingi Laki Tano kwa Kata ya Shanwe na Kata ya Kasokola kwa lengo la kuimalisha uchumi wa Jumuiya ya UWT kwenye Kata hizo pamoja na kutoa Kadi za UWT ili kuendelea kuongeza wanachama .

Pamoja na hayo Mbunge Huyo wa Viti Maalumu Ktika mkoa wa Katavi Martha Mariki amechangia kiasi cha Shilingi Laki Tatu katika kata ya Shanwe kwaajili ya kusaidia ujenzi katika shule ya Msingi Makanyagio.

Hafidhi Masumbuko Diwani wa Kata ya Shanwe ameishukuru Serikali na wabunge wa Mkoa wa Katavi kwa kuendelea kuzisemea changamoto mbalimbali ambazo utatuzi wake umekuwa ukionekana kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye kata hiyo.

‘’Mh Mbuge sisi tunaishuru sana serikali tumemaliza ujenzi wa Madarasa kumi nan ne katika kata hii lakini katika miaka yenu miwili hii unaona haya majengo yote haya tumefanya katika vipindi vyenu wakati ule watoto kuanzia Kidato cha Kwanza nacha pili walikuwa wanakaa chini leo watoto wanachagua wasomee Darasa gani’’

Katika hatua nyingine Diwani Masumbuko amewaasa wanawake wa UWT kata ya Shanwe kutumia fedha hizo walizopatiwa na Mbunge huyo kwa lengo lililokusudiwa la kuimarisha uchumi .

Diwani huyo amechangia  Shilingi Laki Moja kwa wanawake wa UWT Kwenye Kata hiyo kama Sehemu ya Kumuunga Mkono Mbunge Martha kwa Mchango aliowapatia wanawakehao wa UWT  kwenye Kata hiyo.

kwa habari zaidi endelea kufatilia ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages