Mkurugenzi Mtendaji wa wa Taasisi ya Usevya Development [UDESO] Eden Wanyimba akielezea utekezaji wa Mradi kwa washiriki wa kikao hicho. |
Na Walter Mguluchuma,Tanganyika
Taasisi
isiyo ya Kiserikali ya Usevya Development
Sociaty(UDESO ) ya Mkoani Katavi wamefanya tathimi
ya mradi wa AUDIT ACCOUNTABILILITY unatekelezwa katika Wilaya
ya Tanganyika wenye lengo la kuangalia miundo mbinu
inayotokana na taarifa za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)
zilizotolewa mwaka 2017 na kuangalia vitu ambavyo vilivyofanyika hadi
2023
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Usevya Development Sociaty(UDESO ) ya Mkoani Katavi wamefanya tathimi ya mradi wa AUDIT ACCOUNTABILILITY unatekelezwa katika Wilaya ya Tanganyika wenye lengo la kuangalia miundo mbinu inayotokana na taarifa za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) zilizotolewa mwaka 2017 na kuangalia vitu ambavyo vilivyofanyika hadi 2023Washiriki mbalimbali wa kikao hicho wakifatilia kwa makini maelezo ya utekelezaji wa Mradi
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Usevya Development(UDESO) E deni
Wanyimba amesema mradi huu unatekelezwa katika Kata mbili za
Kasekese na Mwese katika Wilaya ya Tanganyika kwa ufadhili wa
shirika la Instute of Public A cconntabilility(WAJIBU).
Mkutano huu wa umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika na umewashiirikisha wajumbe wa kamati ya PETS kutoka katika Vijiji vya Lugonesi, Kasekese.
Waratibu
Elimu Kata , Maafisa watendaji wa Kata hizo Maafisa
Mipango wa Halmashauri,na mwakilishi wa Takukuru wa Wilaya ya Tanganyika walikuwa sehemu ya kikao hicho cha kufanya tathimini ya mradi huo unaotekelezwa katika Wilaya ya Tanganyika.
Wanyimba
amebainisha kuwa mradi huu unafanyika katika shule mbili za
Lugonesi Kata ya Mwese na Kasekase ambao unatekelezwa katika mambo
makuu mawili ambayo ni ni ufatiliaji wa mali za
umma na mfumo wa kuangallia miundo mbinu kufatia
taalifa iliyotolewa na CAG .
Na ndio
maana kwenye mradi huu wakaona wafatilia vitu vingine ambavyo
vimefanyika hadi mwaka 2023 ambapo wameona ni vitu vingi
vizuri ambavyo Serikali wamevifanya miradi
mingi imefanyika kwenye maeneo mbalimbali lakini kwenye mradi huu
wanakamati za PETS hivyo iliviweze kufanya kazi vizuri lazima
washirikiane na mifumo ya Serikali .
Kamati
hizo za Pets zinachaguliwa na kijiji husika unapotekelezwa mradi na
Kijiji kina mamla ya kuwa na kamati hiyo na ndio maana wanatakiwa kufanya
kazi karibu ili zile changamoto zinazopatikana kwenye miundo mbinu
wazilipoti mapema sana ili kuzuia changamoto za miradi zisiweze
kutokea mfano kama fundi anajenga kitu ambacho ni
kinyume cha utaratibu wa ujenzi wakiripoti mapema ili hatua zichukuliwe
mapema za kurekebisha .
Wanyimba
amesema wakati huo huo kamati za Pets wanaweza wakawa wameona jambo
sio zuri linafanywa na walimu au wanafunzi kama utoro wa
mwanafunzi au mwalimu kushindwa kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria
wanaweza kutowa taarifa kwenye vyombo ambavyo vinaweza kuchukua
hatua ambayo Serikali inaona inafaa .
Amefafanua
kuwa toka wameanza kutekeleza mradi huu mwezi wa tatu mwaka huu wameweza
kuonyesha ushirikiano mkubwa na viongozi wa Vijiji na
wameweza kubaini baadhi ya changamoto ya baadhi ya wanafunzi
kushindwa kufika shuleni kipindi cha masika kutoka na mto katika
kijiji cha Lugonesi kujaa maji hivyo kuvuka wao inakuwa ni tatizo na
kusababisha utoro wa reja reja .
Meneja
wa mradi wa kutoka Taasisi ya WAJIBU Moses Kimaro
amesema lengo la mradi huu unaotekelezwa na UDESO
Ni kuisaidia Serikali ili kuleta maendeleo yanayotakiwa kuletwa kwa
wananchi .
Amesema wao kama Wajibu uwajibikaji wanao utaka ni kuangalia ni uwajibikaji wa fedha na rasilimali za umma kwa ajiri ya maendeleo ya Watanzania kwani kama hili likifanyika vizuri kwa fedha kusimamiwa vizuri hata uwajibikaji wa kijamii utakwenda vizuri kwa sababu rasilimali fedha inasimamiwa vizuri na matumizi yatatumika ipasavyo .