SERIKALI YAOMBWA KUVUTA MAJI KUTOKA ZIWA TANGANYIKA KUYAPELEKA KATAVI

 

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi,Martha Mariki akiwa katika kikao Kata ya Ilembo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Na Paul Mathias,Mpanda

Mbunge wa Viti maaalum Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameiomba serikali kuharakisha Mpango wa kuvuta Maji kutoka ziwa Tanganyika ili kuwasaidia wananchi wa mkoa wa katavi kupata huduma ya Maji.

 

Wananchi na wajumbe wa UWT kata ya Ilembo wakiwa katika mkutano na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Katavi.

Mbunge wa Viti maaalum Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameiomba serikali kuharakisha Mpango wa kuvuta Maji kutoka ziwa Tanganyika ili kuwasaidia wananchi wa mkoa wa katavi kupata huduma ya Maji.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanawake wa UWT Kata ya Magamba na Ilembo  Manispaa ya Mpanda Kwenye ziara anayoendelea nayo Kwenye Kata 58 za Mkoa wa Katavi 

’'tunapongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali yetu katika kuimalisha huduma ya Maji Kwenye mkoa wetu wa Katavi lakini Suluhu ya tatizo la Maji Kwa wakazi wa mkoa wetu ni kuvuta Maji kutoka ziwa Tanganyika ambapo ni kilomita 120 Toka hapa’’

Amesema kuwa pamoja na chanzo Cha Maji cha Ikolongo na bwawa la Milala Bado kumekuwa na kususuasua Kwa upatikaji wa huduma ya Maji kupitia  Mgao.

’'natambua vyanzo vyetu vya Maji vya Ikolongo na Bwawa la Milala vyanzo hivi bado havikidhi mahitaji ya wakazi wa mkoa wa katavi na  muarobaini ni kuyatoa Maji kutoka ziwa Tanganyika kama serikali imeweza kuvuta Maji kutoka Mwanza ,Tabora na Shinyanga serikali inashudwa nini kuyatoa Maji kutoka ziwa Tanganyika’’

Katika hatua nyingine amewaomba wazazi na walezi kuzingatia suala la malezi Kwa watoto wao kutokakana na kuibuka Kwa Makundi ya watoto waharifu wanaotokana na jamii zetu na kujiita Majina ya ajabu.

’'wazazi wangu kuna jambo linanisikitisha sana Kuna vikundi vya watoto waharifu wanajiita Damu chafu,Manyingu na mengineyo wazazi tusimame katika malezi watoto Hawa ni wetu Kila mzazi aangalie mwenendo wa mtoto wake watoto hawa wamekuwa na Tabia za kufanya vitendo vya kuvamia watu hasa nyakati za usiku na kuwajeruhi kwa Viwembe na vitu vingine vyenye ncha kali’'

Diwani wa Kata ya Ilembo Joseph Kango’mbe ameishukuru serikali Kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya miradi mbali Katika sekta ya Afya, Maji, Elimu,na Miundombinu Ili kusogeza huduma karibu na wananchi 

Akiwa katika Ziara Hiyo katika Kata za Magamba na Ilembo ameweza Mbunge Martha Mariki ametoa shilingi Laki Tano Kwa Kila Kata Kwa lengo la kuwainua wanawake wa UWT Kwenye Kata hizo pamoja na kutoa kadi za UWT Ili kusaidia kuongeza wanachama wa UWT.

Kwa habari zaidi endelea kutembelea katika kurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages