MWALIMU NSIMBO AKEMEWA KUMBAGUA MWANAFUNZI MWENYE ULEMAVU.

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe akizungumza leo na wananchi wa Kijiji cha Kanoge namba moja.


Na George Mwigulu, Nsimbo.

Mbunge wa jimbo la Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe amewataka walimu kuwa na utu kwa wanafunzi wenye ulemavu ili kujenga mazingira ya kuwavutia wanafunzi hao kwenda shule kusoma na kuondoa tabia ya watoto wenye ulemavu kufichwa majumbani.

Mtoto (Jina tunalo) mwenye ulemavu akiwa amebebwa na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupemba ambapo amesema atahakikisha anapata matibabu sitahiki.

Mbunge wa jimbo la Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe amewataka walimu kuwa na utu kwa wanafunzi wenye ulemavu ili kujenga mazingira ya kuwavutia wanafunzi hao kwenda shule kusoma na kuondoa tabia ya watoto wenye ulemavu kufichwa majumbani.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mbunge huyo katika kijiji cha Kanoge namba moja wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo amepokea malalamiko ya Mkazi wa kijiji hicho,Jackrina James kuwa mtoto wake wa kike(Jina tunalo) mwenye umri wa miaka minne na mlemavu wa kuzaliwa wa kutokuwa na masikio amekuwa akibaguliwa.

Jackrina amemwambia mbunge Lupembe kuwa mtoto wake ambaye ni mwanafunzi wa darasa la awali katika shule ya msingi Tulieni Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi amekuwa akibanguliwa kwa kuitwa majina mabaya (Majina tunayo) na mwalimu anayefahamika kwa jina la Lwila.

Amesema kuwa kitendo cha mwalimu huyo kumwita majina ya ajabu mtoto wake yamekuwa yakimuumiza kwani yeye kama mama hakupenda mwanaye azaliwe akiwa na hali ya ulemavu.

Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kanonge namba moja Kata ya Nsimbo wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe.

Lupembe kutokana na kusikitishwa na kitendo hicho cha kutuhumiwa mwalimu Lwila kufanya ubaguzi licha ya kumtaka Diwani wa Kata  Nsimbo na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kanoge namba moja kufutilia suala hilo haraka pia amewataka walimu sio kuwa na upendo tu bali kuzingatia maadili yao ya kazi.

Vilevile mbunge huyo kwa kuguswa na hali ya mwanafunzi huyo amemchukua kwa ajili ya kuhakikisha anamsaidia kupata matibabu yatakayowezesha kuwa na uwezo wa kusikia zaidi.

Nao baadhi ya wakazi wa kijiji hicho,France Zachal amemshukuru mbunge wa jimbo hilo kwa kuweza kumchukua mtoto huyo kwa ajili ya matibabu,amesema kuwa moyo wa upendo ambao amekuwa akiuonesha kwa wanajimbo la Nsimbo sio wa kutiliwa shaka na watakuwa pamoja naye daima.

Frances amesema kuwa walimu wenye tabia za ambazo zinakwenda kunyume na maadili yao ya kazi wanapaswa kijitafakari na kutabua kuwa kazi ya kuwa mwalimu ni taaluma na pia ni wito hivyo wanapaswa kuwa na upendo kwa wananfuzi sio wenye ulemavu pekee bali wote.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages