PINDA SERIKALI KUANZISHA BENKI YA ARDHI NCHINI.


Naibu Waziri wa Wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya Makazi,Geofrey Pinda (Mb) akizungumza leo na watumishi wa idara ya ardhi wa Mkoa wa Katavi katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda.

Na George Mwigulu, Katavi.

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi inampango wa kuanzisha benki ya ardhi kila mkoa nchini kwa ajili ya kusaidia kutatua migogoro ya ardhi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza leo ofisini kwake wakati  Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Geofrey Pinda (Mb).

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi inampango wa kuanzisha benki ya ardhi kila mkoa nchini kwa ajili ya kusaidia kutatua migogoro ya ardhi.

Amesema hayo leo Naibu Waziri wa wizara hiyo, Geofrey Pinda (Mb) akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Katavi wakati akizungumza na watumishi wa idara ya ardhi wa mkoa huo katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.

Naibu waziri Pinda amesema migogoro mingi iliyopo kwenye wizara ya ardhi inatokana na ongezeko la watu ikiwa ardhi hiyo haiongezeki.

Pinda ameeleza kuwa watumishi wa idara ya ardhi kwa mazingira ya kawaida wamekuwa wakikimbia wateja wenye matatizo ya viwanja wanapokuja kutafuta huduma kwa sababu hakuna eneo la ardhi mbadala ambapo mtu anaweza kupelekwa kwa kuwa wamemaliza maeneo yote.

Amefafanua kuwa Benki ya ardhi itaweka akiba ya maeneo kwa idara ya ardhi na pindi linapotokea tukio lolote la mtu kuuziwa  juu ya kiwanja cha mtu mwingine ataweza kupewa kiwanja cha eneo lingine.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,Abas Rugwa (Kushoto)akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph (Kulia) wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo na Makazi,Geofrey Pinda (Mb).

“inapotokea incident mtu amepangishiwa kiwanja juu ya kiwanja huna nafasi hata ya kumuona matokeo yake wanakwenda kurudikana kwa Ma_Das na Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuomba msaada,hata kama wataombwa hawa watakuita tu na wanapokuita lazima uwe na back up ya majibu tutakayoweza kusaidia serikali kuondoa migogoro” Amesema Naibu Waziri huyo.

Naibu waziri huyo amesema kuwa kama wizara  wanampango wa mradi wa matumizi bora ya ardhi vijijini utakapunguza migogoro ya ardhi kwa sababu utabainisha matumizi yaliyopo kwenye maeneo.

Ameeleza licha ya kuwa kunachangamoto kwenye eneo la fedha  ambalo litasaidia kwenye utekelezaji wa vijiji 10,000 nchini kwenye mradi wa matumizi bora ya ardhi lakini kiasi cha fedha Bil 40 zitatumika kupima vijiji ambavyo havitakuwa vyote.

Aidha kutakuwa na zoezi nchi nzima la kurudia michoro ya ramani kupitia mradi wa korea ambapo utaenda kuhuwisha ramani na kuhakiki ongezeko lilipo kwenye matumizi ya ardhi kwenye ramani.

“Tuna ramani za muda mrefu sana ambazo hazina kumbukumbu sahihi kutokana na mabadiliko ya ardhi…sasa ramani tuliyo nayo inasoma labda Kasekese ni hifadhi lakini kumbe sisi Kasekese tulishaitoa na imerudi kwenye matumizi ya wananchi” Amesema Pinda huku akibainisha kuwa hadi sasa wamepuguza maeneo ya hifadhi na kuwarudishia wananchi.

Watumishi wa Idara ya ardhi Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye ukumbi wa manispa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye kikao kazi na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi,Geofrey Pinda (Mb). 

Katika kutatua changamoto ya vifaa vya vipimo vya ardhi,Naibu waziri huyo amesema kuna fedha Bil 7 zilitengwa za utawala lakini bunge halikukubaliana na kiasi hicho cha fedha  zilizotengwa katika mfuko wa tume ya ardhi  ambapo waliongeza Bil 25 ikiwa Bil 5 zitachangwa na TAMISEMI kufikia Bil 30 zitakazoongeza uwezo kwenye mfuko wa tume ambapo vifaa hivyo vitanunuliwa na kupunguza uhaba uliopo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mridoko amesema kuwa takribani ya migogoro 60 ya ardhi iliyokuwa Mkoa wa Katavi chini ya kamati ya Mawaziri nane imeshaanza kutekelezwa.

Mrindoko amesema kuna migogoro mingine ambayo iko nje ya kamati ya mawaziri nane  nayo ameshaanza kuitatua kwa sababu ya kuendelea kukua kwa mkoa migogoro itaendelea kuwepo lakini watatatua kwa wakati.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages