Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda Tausi Ramadhani akizungumza na wanawake wa UWT kwenye Mkutano wa Baraza la UWT wilaya ya Mpanda. |
Na Paul Mathias,Mpanda
Wanawake wa Jumuiya ya UWT wilaya
ya Mpanda wameaswa kuendelea kuhamasisha wanawake kujiunga na jumuiya hiyo ili
kuongeza nguvu ya pamoja katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Jumuiya ya wanawake ya Chama cha Mapinduzi CCM UWT wilaya ya Mpanda wameaswa kuendelea kuhamasisha wanawake kujiunga na jumuiya hiyo ili kuongeza nguvu ya pamoja katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Leah Gawaza akiwahutubia wanawake wa UWT Wilaya ya Mpanda katika baraza la UWT lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mpanda
Akiwa hutubia wanawake wa
Jumuiya hiyo Katika Baraza la UWT Wilaya ya Mpanda Mwakilishi wa Mkuu wa hilo
Leah Gawaza ambae ni Afisa Tarafa ya Misunkumilo amesema kuwa wanawake kupitia
UWT wanao wajibu wa kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanachama ili kutengeneza
mazingira mazuri katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.
‘’muda siorafiki tunakimbizana
sana na uchaguzi wa Mwakani tusimwache mtu hata mmoja nyuma kila kura moja
inathamani ndunguzangu sasa hivi tunaenda kwenye Boksi la kura kwenye Boksi
tunahitaji watu ili kuhakikisha tunapata ushindi hivyo akina mama tuhakikishe
tunawaingiza watu wengi zaidi’’
Katika hatua nyingine amewapongeza UWT kwa kuwa na mikakati mbalimbali ya kujiinua kiuchumi kupitia vikundi mbalimbali hali ambayo inasaidia jumuiya hiyo kujitegemea kiuchumi
Awali akisoma taarifa ya UWT
Wilaya Kwaniaba ya Katibu wa Jumuiya hiyo Grace Abisai amesema kuwa chama hicho
kimendelea kuongeza wanachama kupitia usajili mtandaoni.
‘’kwa kipindi cha January 2023
hadi June 2023 kumekuwa na ongezeko la wanachama ni 4199 na mpaka sasa
waliosajiliwa kwenye mfumo wa Tehama ni wanachama 2354’’
Amesema jumuiya hiyo inamipango mbalimbali ikiwemo kujenga nyumba ya Mtumishi wa UWT Wilaya ya Mpanda kuandaa semina na mafunzo kwa wanachama na kuanzisha miradi ya kiuchumi kuanzia ngazi ya Kata hadi wilaya na kuendelea kuongeza wanachama kupitia mfumo wa Tehama.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya
Mpanda Tausi Ramadhani amesema ajenda yao kubwa kwa sasa ni kushinda katika
uchaguzi wa Serikali za mitaa Mwakani pamoja na uchaguzi mkuu 2025
Sebastiani Kapufi Mbunge wa
Mpanda Mjini Akitoa salamu kwa wanawake wa Jumuiya hiyo amesema UWT ni nguzo mhimu katika Wilaya ya Mpanda
kwakuwa mara nyingi Jumuiya hiyo imekuwa imara katika kufanikisha Mambo
mbalimbali ndani ya chama na Jumuiya hiyo kwa ujumla.
Jumuiya ya wanawake ya Chama cha Mapinduzi UWT inajumla ya wanachama 14,898 .