Na George Mwigulu,
Tanganyika.
Baadhi ya wanawake katika wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wamepewa usawa wa kijisia kwenye utekelezaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kukuza hali ya upatikanaji sawa wa rasilimali na fursa bila kujali jinsia.
Afisa
ardhi wilaya ya Tanganyika,Mussa Yohana amesema hayo leo wakati wa kukabidhi
hati Milki za kimila katika kijiji cha Vikonge kata ya Tongwe ambapo utekelezaji wa
mradi huo umefanikiwa kuboresha milki za ardhi bure kwa kupima mashamba na viwanja 3460 na kutoa
hatimilki 1337 kwa wananchi.
Yohana
ameeleza juhudi za kuhakikisha usawa wa kijisia kwenye upatikanaji sawa wa
rasilimali wameweza kutoa fursa sawa kwa
jinsia zote kushiriki ambapo kati ya hati 1337,hati 481 sawa na asilimia 36
zimesajiliwa kwa majina ya njinsi ya kike.
Wanawake kushiriki katika zoezi la umilikishaji kulikuwa na changamoto mkubwa kwa kuwa na mfumo dume ambao jamii inaamini kuwa kwenye haki ya kumiliki ardhi ni mwanaume lakini kwa kutumia sheria namba 4 na 5 ya mwaka 1999 imetoa fursa kwa mwanamke nafasi sawa na mwanaume ya kumiliki ardhi.
Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi,Mussa Yohana akizungumzia jitihada ambazo zimewafanya kufanikiwa kutoa hati Milki za kimila kwa wanawake wa wilaya hiyo. |
“sheria hii imetoa fursa ambayo tumeitumia katika utekelezaji wa mradi huu ambapo tumetoa hamasa kwa wanawake kushiriki na kutafasiri sheria ili wapate fursa ya kumiliki ardhi sawa na wanaume” amesema Afisa wa ardhi huyo.
Kutokana
na wanawake kutengwa kwenye umilki wa mali kwenye ngazi ya familia wamefanikiwa
kuhamasisha umilki wa pamoja baba na
mama kwa umoja wao kushiriki katika zoezi la upimaji wa vipande vyao vya ardhi
kwa kupigwa picha pamoja na hati kutoka kwa majina ya mawili ya mume na mke.
“tumetoa pia fursa kwa mwanamke ambaye kimsingi ametafuta ardhi kwa nguvu yake naye amehamasishwa bila kuingiliwa na mtu mwingine kwenye maamuzi naye ameweza kushiriki kwenye upimaji na kupewa hati milki kwa jina lake”.amesema Yohana.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Jane Goodall,Dkt Kasukura Nyamaka amesema taasisi inashirikiana na halmashauri ya wilaya
ya Tanganyika,Uvinza na Kigoma kuandaa matumizi ya ardhi ya vijiji na mipango ya
matumizi ya ardhi ya wilaya.
Mradi
wa LCWT umeziwezesha serikali za vijiji kwa kushirikiana na halmashauri za
wilaya kuandaa,kutathimini na kurejea mipango ya matumizi ya ardhi kwa vijiji
53 kata 74 imetekelezwa na taasisi miradi mingine ya miaka ya nyuma kati ya mipango
ya ardhi ya matumizi ya ardhi ya vijiji 53 imerejewa,mipango 46 imewasilishwa
tume ya taifa ya mipango ya matumizi ya ardhi.
Dkt Nyamaka amesema kuwa lengo la Jane Goodall la kufadhili upimaji wa vipande vya ardhi na utoaji wa hati Milki za kimila ni kuongeza ushirikishwaji wa wanawake na vijana kwenye masuala ya umiliki na usimamizi wa rasilimali ardhi ili kuongeza chachu ya uhifadhi wa maliasili za misitu na wanyamapori hasa Sokwemtu.
Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi,Geofrey Pinda akikabidhi hati Milki ya kilima kwa mume na mke ambapo hati hiyo inaumilki wa pamoja. |
“taasisi ya Jane Goodall kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Tanganyika,Uvinza na Kigoma tumefanikiwa kupima na kukusanya taarifa za vipande 13,105 katika vijiji 12 ambapo tunatarajia watu 13,749 watanufaika na upimaji huo ikiwa vijana wa kike 1,218 na wanawake watu wazima 4,092” Amesema Dkt Nyamaka.
Eliata
Korinalio,Mkazi wa Kijiji cha Vikonge Wilaya ya Tanganyika ambaye ni mnufaika
wa kuwepa hati milki ya kimila ameishukuru serikali kwa kushitikiana na taasisi
ya Jane Goodall kwa kufanikisha adhima yao ya kumiliki ardhi.
Amesema
hati hizo zitawasaidia kama dhamana ya kupewa mikopo ya fedha ambazo
zitaboresha mitaji kupitia biashara wanazofanya.