Na Walter Mguluchuma,Katavi .
Mkoa wa Katavi
uko tayari kushiriki kikamilifu kwa moyo mkunjufu
kuhakikisha mpango wa dira ya
maendeleo wa mwaka 2050 unafanikiwa kwa musitakabari mzuri na maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Viongozi mbalimbali wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa semina ya maandalizi ya uhamasishaji wa mpango wa dira ya maendeleo ya 2050 |
Mwanamvua
amebanisha kuwa tulikuwa na dira ambayo inaishia mwaka 2025 na sasa
tunakwenda kwenye dira ya 2050 anaamini
kuwa semina hiyo itasaidia kujenga uwelewa kwa viongozi wote wa Mkoa na Wilaya na wadau wote
kuhusu mchakato mzima wa
maandalizi ya dira ya dira ya maendeleo
ya 2050.
Amewaomba
wananchi na viongozi wote wa Mkoa wa Katavi
kushiriki kwa pamoja ili kuwa na uwelewa wa pamoja na kwa
kutambua kila mtu majukumu yake ni yapi
katika kuandaa mpango huo muhimu kwa Serikali na wananchi wote kwa ujumla .
Amebainisha
kuwa Mkoa wa Katavi wapo tayari kwa kazi iliyoko mbele ya kuhakikisha wananchi wote na makundi mbalimbali wanapata uwelewa kama
ambao waliopata wao wa kuhusiana
na dira ya 2025 ambayoinaelekea
ukingoni na dira
mpya ya 2050 inayokwenda kuandaliwa .
Mrindoko alisema
Katavi wapo yatari wapo tayari kwa asilimia mia moja kuhakikisha jambo
hilo muhimu hapa nchini nilifatiwa bila shida wala kikwazo chochote
kile hivyo watashiriki kwa ukamilifu
kwenye jambo hilo .
Nae Victoria
Mariale kiongozi wa timu ya
uhamasishaji wa mchakato wa maandalizi ya dira ya maendeleo ya 2050 kwa mikoa ya Katavi Rukwa ,
Kigoma , Tabora na Singida amesema lengo kubwa la uhamasishaji ni
kuendeleza dhama kubwa kwa wananchi kushiriki kupanga maendeleo yao ili kupanga Tanzania waitakao wao katika
miaka 25 ijayo .
Kwa hiyo mchakato
wa kutengeneza dira ya maendeleo ya Taifa ulizinduliwa tarehe 3
mwezi wa nne na Makamu wa Rais Dk
Philipo Mpango na alisisitiza
ushirikishwaji mpana wa Watanzania kuamua
Tanzania waitakayo kwa hiyo
wao wapo kuhakikisha wanashiriki
kutowa maoni yao kutengeneza dira ya maendeleo .
Amesema mwamko
wa washa hiyo umekuwa ni mkubwa hivyo wanaamini na wananchi watashiriki kwa
wingi kwa kuwa viongozi wengi wamefikiwa kwani lengo kubwa ni kuhakikisha kila
Mtanzania anajua kuna mchakato wa kutengeneza dira na anatowa maoni yake .
Padre
Anacretus Bafumkeko wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Mpanda ameshauri uwepo
wa makini kwenye mchakato huu kwani
kunaweza kukawepo watu wachache ambao wanaweza kufanyamambo kiujanja ujanja nap engine kukwamisha mwelekeo wa dira ambayo tunataka itusaidie kuendelea na kufikia maendeleo endelevu .