WANANCHI UGALLA WAIPA HEKO SERIKALI UJENZI KITUO CHA AFYA

 

Wananchi wa Kata ya Ugalla wakiwa  Katika picha ya Pamoja na Mbunge Mbunge Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki baada ya Kutembela Kata ya Ugalla

Na Paul Mathias,Nsimbo

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameishukuru serikali Kwa kutoa fedha Shilingi Milioni 590 Kwaajili ya kufanikisha ujenzi wa Kituo Cha afya Ugalla Halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi.

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki[ Katikati]akiwa na Viongozi wa UWT Wilaya ya Mpanda Pamoja na Kamati ya Utekelezaji ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi wakipokelewa na wanawake wa UWT Kata ya Ugalla

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ameishukuru serikali Kwa kutoa fedha Shilingi Milioni 590 Kwaajili ya kufanikisha ujenzi wa Kituo Cha afya Ugalla Halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi.

Akizungumza na Wananchi katika Kijiji Kasisi Kata ya Ugalla wakati wa ziara ya kutembelea Kata za Mkoa wa Katavi.

Amesema kuwa Kitendo Cha serikali kujenga Kituo Cha Afya Ugalla utakwenda kuwakomboa wananchi kupata huduma karibu na adha ya kupata Huduma za Afya katika Kituo Cha Afya Kanoge ambacho kipo mbali kutoka Kijiji Cha Ugalla.

Muonekano wa Kituo cha afya Ugalla ambacho kimejegwa na Serikali kikiwa na Jengo la Mamama na Mtoto pamoja na Maabara

"serikali imedhihilisha kuwa inaadhima ya kuhakikisha wakazi Hawa wa Ugalla wanapata huduma za Afya hapa hapa Ugalla serikali yetu imeleta fedha Shilingi Milioni 590 Kwaajili ya ujenzi wa Kituo Cha Afya na Leo kituo kimejengwa na huduma zinatolewa"amesema Mbunge huyo.

Ameeleza kuwa Maendeleo yanayoonekana katika Kata hiyo na Jimbo la Nsimbo Kwa ujumla inatokana na kuchagua Viongozi wenye Uchu wa kuwaletea wananchi Maendeleo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna lupembe.

 "Haya maendeleo mnayoyaona ndugu Wana Kasisi na Wana Ugalla yanatokana na kuchagua Viongozi wenye Uchu wa maendeleo wakiongozwa na Mh Anna lupembe na Diwani wetu Halawa"

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi ,Martha Mariki[ Kulia] akipata maelezo kutoka kwa Diwani wa Kata ya Ugalaa Charles Halawa juu ya Miradi kadhaa inayotekekelezwa na serikali Katika kata ya Ugalla

Ameishuru serikali ya Awamu ya Sita Kwa kuendelea kuleta fedha za maendelea katika mkoa wa katavi Ili wananchi waendelee kupata huduma na kuwa na usitawi mzuri wa kimaisha katika maisha Yao ya kila siku.

Shija Malembeka mkazi wa Ugalla amesema kuwa walikuwa na ndoto ya siku nyingi kujengewa kituo cha Afya kwakuwa walikuwa wanapata changamoto ya kupata Matibabu haraka lakini kwa sasa wananufaika na ujenzi wa Kituo hicho cha Afya Ugalla

Diwani wa Kata ya Ugalla Charles Halawa akizungumza na wananchi wa Kata ya Ugalla 

Malembeka ‘’anasema zamani tulikuwa tunapata shida ndugu mwandishi Mgojwa kumtoa hapa ugalla hadi Kanoge ilikuwa inatuchukua muda mrefu kutokana na umbali hadi kufika huko tunawashukuru viongozi wetu kwa hili’’

Kwa upande wake Suzana Kwabi amesema maendeleo yanayofanywa na serikali Katika Kata ya Ugalla yanawapa matumaini ya kuendelea kuiunga mkono serikali katika kuungamkono miradi kupitia nguvu kazi.

‘’Mimi nikisikia serikali inaleta Mradi nipo tayari hata kuchimba Msingi na visiki ili mradi huo utunufaishe amesema ‘’Suzana

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ugalla ambae ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Charles Halawa amesema kilio Cha Wana ugalla kilikuwa ni Kupata Kituo Cha Afya ambacho tayari serikali imejenga.

'hatuna Cha kumlipa mama Samia zaidi ya kusema Asante Kwa mradi huu zamani Ili mlazimu mkazi wa Ugalla kupata huduma Kituo Cha Afya Kanoge lakini Kwa ujenzi juu serikali imewatendea haki wananchi Hawa"amesema Halawa 

 

Katika hatua nyingine Halawa ameishukuru serikali Kwa kuendelea kuleta Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwenye sekta za Elimu,Afya, Miundombinu na uwezeshaji wanawake,vijana na walemavu Kupitia mikopo ya Halmashauri.

Ziara ya Mbunge wa Viti maalumu katika Mkoa wa Katavi inaendelea katika Jimbo la Nsimbo ambapo Mbunge huyo akiwa katika Kata za Ugalla na Litapunga ametoa shilingili Laki Tano Kwa Kila Kata Kwa Wanawake wa UWT wa Kata za Ugalla na Litapunga Ili waweze kujikwamua kiuchumi.

 Pamoja na kutoa Kadi za UWT Ili jumuiya Hiyo iendelee kuiamrika zaidi na kuendelea kuwa nguzo ya chama Cha Mapinduzi CCM.

Kwa habari zaidi endelea kutembelea ukurasa wetu wa 

kataviclub.blogspot.com 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages