UJENZI WA SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA KUNUFAISHA TABAKA LA CHINI MPANDA.

Haidary Sumry,Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi akizungumza wakati wa ziara ya kikazi  ya kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo.Ambapo kwenye ziara hiyo madiwani wote wa Manispaa hiyo waliihudhuria.

Na George Mwigulu, Mpanda.

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi inatekeleza mradi wa ujenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza (English Mqedium school) kwa ajili ya kuwasaidia wazazi na walenzi ambao wanania ya kusomesha watoto kwenye shule binafsi lakini wameshidwa kumudu gharama kubwa  za kusomesha.

Moja ya Jengo la Darasa ambalo English Medium School inajengwa katika eneo la shule ya msingi Misukumilo.

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi inatekeleza mradi wa ujenzi wa shule ya mchepuo wa kiingereza (English Medium school) kwa ajili ya kuwasaidia wazazi na walenzi ambao wanania ya kusomesha watoto kwenye shule binafsi lakini wameshidwa kumudu gharama kubwa  za kusomesha.

Ujenzi wa mradi wa shule hiyo unatekelezwa katika eneo la shule ya msingi Misukumilo kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya Manispaa ya Mpanda ambapo fedha Mil 260 zinatumika kukamilisha mradi huo.

Haidary Sumry,Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda akiongozana leo na madiwani wote kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo amesema kuwa shule hiyo itakuwa na kiwango cha juu cha utoaji elimu ya msingi ikizingatiwa ni mali ya serikali.

Msitahiki Meya huyo ameeleza kuwa licha ya lengo ni kutibu matamanio ya wananchi wa uchumi wa chini kuwezesha watoto wao kusoma English Medium School kutokana na unafuu mkubwa wa ada utakao kuwepo lakini shule hiyo itakuwa ni sehemu ya kitega uchumi kipya kitakacho ongeza mapato ya manispaa hiyo.

Msitaki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Haidary Sumry akikagua moja ya shimo la choo katika shule ya msingi Kawalyowa.

Madiwani  wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakisikiliza taarifa ya Mwl festo Malekela wa shule ya msingi Misukumilo ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa mradi wa shule ya mchepuo wa kiingereza. 

“ni shule ambayo itakuwa na mchepua wa kiingereza lakini ambayo itakuwa na gharama nafuu zaidi tofauti na shule za private hivyo itawasaidia wananchi wa kati sio matajiri ambao walitakiwa kulipa Tsh 150,000/- kwa kila robo ili asome kwa shule ya English Medium School  akawa anashidwa kwa sababu labda kwenye private ni Tsh 400,00/= au Tsh 500,000/= sasa watapata majawabu ya wototo kupata elimu kwenye shule ya serikali  kwa ghrama nafuu” Amsema Sumry.

Amewaomba wazazi na walezi kuchangamkia fursa hiyo pindi shule itakapokamilika kujengwa akiwahakikishia kuwa huduma za shule hiyo zitakuwa bora zaidi ili kulinda heshima ya serikali.

Kaltas Mangwangwa,Diwani wa viti maalumu Manispaa ya Mpanda amesema ujenzi wa mradi wa English Medium School ni matokeo chanya ya ziara ya madiwani wa manispaa hiyo waliyoifanya mwaka 2021/22 jijini Mbeya baada ya kuona jiji hilo limefanikisha kubuni mbinu mpya ya kukusanya mapato.

Diwani huyo amefafanua kuwa kuanzishwa kwa shuleni hiyo ni mwanzo tu bali kama serikali ya Manispaa ya Mpanda wataendelea kujenga shule za namna hiyo kwa masirahi ya wananchi wa uchumi wa chini na kati.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa shule hiyo mbele ya Meya na Madiwani,Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Misukumilo,Festo Malekela  amesema kuwa ujenzi wa mradi wa shule ya mchepuo wa kiingereza unahusisha vyumba nane vya madarasa,ofisi mbili za walimu,matundu 12 ya vyoo na jiko kwa thamani ya Mil 260 ambapo umefikia asilimia 85.

Sehemu ya majengo ya madarasa ya shule ya msingi yanayojengwa kupitia mradi wa boost katika eneo la Ilembo.

Kituo cha Afya Kazima kilichopo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambavyo vimekaguliwa na Madiwani.

Mwl Malekela amesema licha ya mafanikio hayo kuna changamoto za upatikanaji wa maji,hata hivyo ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa iliomba kuuganishiwa maji ya bomba pamoja na kufuta tenki la kuhifadhia maji ya akiba hali iliyosaidia kupunguza changamoto.

Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda wakizungumza kwa wakati tofauti,Sophia Christopher Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa  ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuanza utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa shule ya mchepuo wa kiingereza kwani hakutegemea kama viongozi watakuwa na maono hayo makubwa.

Sophia ameeleza kuwa wao kama wazazi ni fursa kubwa wataitumia kuhakikisha watoto wanapata elimu ya kiwango cha juu hasa watoto kuongeza ufanisi wa kuongea lugha ya kiingereza ambayo inatumika zaidi kwenye elimu ya sekondari.

Aidha,Madiwani katika ziara hiyo wameweza kukagua ukarabati wa hosptali ya Manispaa ya Mpanda,Ujenzi wa shule ya msingi Kawajese,Kazima,Kituo cha afya Kazima,Ujenzi wa jengo la utawala na matundu 20 ya vyoo eneo la Kawalyowa na Ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari ya wasichana Mpanda ambapo madiwani hao walilidhishwa na ujenzi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages