WABUNGE VIJANA WAUNGA MKONO UWEKEZAJI WA BANDARI

 

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki akizungumnza na wanawake wa UWT Pamoja na viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda.

Na Paul Mathias,Mpanda

Wananchi katika mkoa wa Katavi wametakiwa kutokuwa na hofu juu ya Mpango wa serikali wa kutaka kuingia mkataba wa Mwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam kutoka kampuni ya Dp World ya nchini Dubai.

 

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki [Kulia]akiwa na Mbunge wa Vijana kutoka mkoa wa Kigoma Sylivia Sigula  [kushoto] wakiwa katika mkutano na wanawake wa UWT kata ya Kashaulili Wilaya ya Mpanda.

Wananchi katika mkoa wa Katavi wametakiwa kutokuwa na hofu juu ya Mpango wa serikali wa kutaka kuingia mkataba wa Mwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam kutoka kampuni ya Dp World ya nchini Dubai.

Akizungumza na Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi UWT Katika Kata ya Kashaulili na Makanyanyagio Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki amesema.

Mpango huo huo wa serikali wa kutaka kuingia Mkataba wa Mwekezaji katika Bandari ya Dar es salaam utaongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Bandari ikiwemo kuongeza mara dufu ukusanyaji wa Mapato katika Bandari Hiyo.

‘’ndugu zangu akina mama wenzangu wa mkoa wa katavi kumekuwa na upotoshaji mwingi kuhusu suala la Bandari hapa nchini nia ya serikali siyo kuuza Bandari Bali ni kuweka Mwekezaji kwa kushirikiana na serikali ambae atasimamia vizuri ufanisi na utendaji kazi wa Bandari kwa kisasa zaidi kulingana na nyakati hizi za maendeleo ya utandawazi’’

Amesema kuwa uwekezaji wa Bandari ya Dar Es salaam utapunguza Adha ya wafanya biashara kusubilia mizigo yao Kwa muda mrefu kupakua mizigo yao ya bidhaa mbalimbali.

‘’Wafanya biashara huwalazimu kusubilia kupakua mizigo yao Kwa muda mrefu pale Bandarini uwekezaji wa Bandari hii utaenda kutatua tatizo hilo Kwa wafanya biashara kutumia muda mfupi kuchukua mizigo yao kutokana na Technolojia itakayo kuwa inatumika kwenye Bandari’’

Kwa upande wake Mbunge wa Vijana Taifa  kutoka mkoa wa Kigoma Sylivia Sigula akiwa katika Mkutano huo amesema wananchi wawe na imani na serikali yao kuhusu uwekezaji wa Bandari.

‘’watanzania na wanakatavi Kwa ujumla serikali ipo makini kuhusu suala hili Kuna baadhi wanasema Bandari inauzwa naomba niwaambie Bandari haiuzwi’’

Katika hatua nyingine amewaomba wananchi na Wanachama wa chama Cha Mapinduzi CCM kuendelea kumuunga mkono Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia wananchi Kwa kuwaletea Maendeleo.

Katika Mkutano huo Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ametoa shilingi laki Tano kwa kila ikiewemo kata ya Makanyagio na kashaulili Kwa leongo la kuwainua wanawake wa UWT Ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mbunge wa Vijana Taifa kutoka Mkoa wa Kigoma Sylivia Sigula cilivia Mbunge anaetokana na Vijana kutoka mkoa wa Kigoma ambae alihudhuria mkutano huo ameto shilingi Laki mbili Kwa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Mpanda UWT Ili kusaidia ujenzi wa Nyumba ya Mtumi wa UWT Wilaya ya Mpanda.

Ikumbukwe kuwa Mbunge Martha Mariki yupo katika zaiara ya Kutembelea kata zote za mkoa wa katavi zipatazo 58 Kwa leongo la kuzungumza na wanawake wa UWT Mkoa wa Katavi na kuwaelezea mazuri yanayofanywa na serikali ya Awamu ya Sita ya Dk Samia Suluhu Hassan

 

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages