Na George
Mwigulu,Nsimbo.
Wananchi wa kitongoji cha Songambele Kijiji cha Tumaini Kata ya Itenka halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wamekiri kuwa matatizo ya utolo shuleni na mimba za utotoni zitakoma baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Makomelo.
Mbunge wa jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe akikangua leo ujenzi wa shule ya msingi Makomelo. |
Ujenzi wa shule hiyo unatekelezwa chini ya mradi wa Boost ambapo fedha Mil 561 zinatumika kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa 16 sambamba na vifaa vya samani kama vile madawati.
Masolwa
Malubalo,Mkazi wa kitongoji cha Songambele ameeleza wamekuwa na matatizo ya
watoto wao kwenda shule umbali wa zaidi ya km tisa jambo ambalo licha ya juhudi
kubwa za kuchangia chakula mahala pakusomea lakini bado watoto wao walishindwa
kumudu umbali hao.
Malubalo amesema kuwa umbali huo umekuwa ni chanzo cha watoto wao kushindwa kufika shule na kuwa watolo sugu sambamba na baadhi ya watoto wao wakike kupata vishawishi kwa wanaume waovu na kupatiwa ujauzito na kushindwa kuendelea na masomo.
Pili
Deus anasema walichoshwa na matatizo hayo ambapo waliweza kuchanga fedha ambazo
ziliwawezesha kupata eneo lenye thamani ya Mil 4.8 na kuanza kubeba mawe ili
kuanza ujenzi wa shule.
Anafafanua
kuwa Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe ndio aliwaambia kuwa kwa kuwa
ameona juhudi zao atawapigania ili hakikisha wanapatiwa fedha ambazo
zitawezesha ujenzi wa shule hiyo.
“hatukutarajia baada
ya kuambiwa Mil 561 zimeletwa kwa ajili ya ujenzi wa shule yetu,Tunamshukuru
Mbunge Anna na serikali ya halmashauri ya wilaya ya Nsimbo chini ya Mkurugenzi Mohamed kwa kufanikisha
hili” amesema
Pili.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe amesema kuwa serikali ya awamu ya sita lengo lake ni kutengeneza mazingira bora na rafiki ya wanafunzi kusomea ili kujenga taifa la watu wasomi.
Ambapo amesema ujenzi wa shule hiyo utakwenda kuondoa adha ambayo wanafunzi wa maeneo hayo wamekuwa wa kipata kwa muda mrefu ikiwa nia yake ya kujenga shule mpya ya sekondari akiiweka wazi kwenye kitongoji hicho.Lupembe
amesema kuwa mradi wa boost umekuja ukiwa umejitosheleza,hivyo ametoa maagizo
kuwa hata furahishwa kuona wananchi wanachangishwa fedha kwa ajili ya madawati.
Naye
Diwani wa Kata ya Iteka,Joseph Laurent amesema ujenzi wa shule katika eneo hilo
umelenga kuwapunguzia watoto umbali wa kwenda masomoni ikiwa pamoja na
kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi katika shule ya msingi Iteka A ambapo zaidi
ya wanafunzi 3600 wako hapo.