Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akiwa katika ziara ya kukagua Ukarabati wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo kwa waandishi wa habari hospitali hapo |
Na Paul Mathias,Mpanda
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila yusuph amemwagiza mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda kuhakikisha ukarabati wa Majengo,na Ujenzi wa Majengo Mapya Katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda unakamilika ifikakapo 30/10/2023.
Moja ya jengo jipya lililojengwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambalo mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amefika na kufanya ukaguzi |
Maelekezo
kezo hayo ameyatoa alipotembelea hospitalini hapo kukagua mwenendo wa baadhi ya
majengo unaoendelea kwenye hospitali hiyo
ambapo serikali imeleta fedha shilingi milioni 900 ili kukarabati miundo
mbinu hiyo ya majengo ya hospitali ya Manispaa ya Mpanda.
‘’Nimwagize
mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda kuhakikisha ujenzi huu unakamilika ifikapo
tarehe 30/10/2023 ujenzi uwe umekamilika wodi zote ambazo zinajengwa ziwe
zimekamilika na majengo mapya amabayo yanajengwa yawe yamekamilika’’ amsema
Jamila yusuph mkuu wa wilaya ya Mpanda
Jengo la mionzi katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda likiwa katika hatua za mwisho kukamilika tayari kwa kuanza kufanya kazi |
Katika hatua nyingine ameipongeza Serikali ya kwa kuleta fedha zaidi Milioni 900 kwaajili ya ukarabati wa Majengo ya hospitali hiyo pamoja na ujenzi wa Majengo mapya hali ambayo itasaidia upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Mkuu
huyo wa Wilaya ya Mpanda ameridhishwa na ukarabati wa hospitali hiyo na
kuwaomba wasimamizi kuendelea kufanya kazi hiyo ili kumaliza ujenzi huo kwa
wakati naili huduma zianze kutolewa
kwenye majengo hayo.
Mkuu
wa wilaya ya Mpanda ametoa rai kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo kuendelea
kuwahudumia Wagojwa kwa weledi kwakuwa serikali inaendelea kuboresha miundo
mbinu ya sekta ya afya kwa Vitendo.
Mganga
mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dk Paul Lugatha amesema majengo yaliyo
kalabatiwa ni ukalabati wa jengo la wanawake [wodi ya upasuaji] ambalo
limetengewa Milioni 54,ukarabati wa jengo la wanawake[Medical word
]iliyotengewa Milioni 56 ukarabati wa jengo la wanaume milioni 56 na jengo la
wanaume la upasuaji lililotengewa
milioni 54
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph [kushoto]akiwa katika ukaguzi wa Majengo yanayokarabatiwa na kujengwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda |
Dk Lugatha amesema kuwa majengo mengine yanayoendelea kukarabatiwa wa Wodi ya watoto iliyotengewa milioni 66 jingine ni ukarabati wa Jengo la Bima lilitengewa zaidi ya Milioni 5.
Onolata
Mgawe mkazi wa Manispaa ya Mpanda ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa
kufanya ukarabati wa hospitali hiyo ili wananchi wapate huduma katika mazingira
mazuri.
''kunamabadiliko
Makubwa sana sasa hivi ukarabati huu wa Majengo haya hata kama unamgojwa
ukimfikisha hapa anajihisi kupona amsema'' Onolata.