Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo. |
Na Paul Mathias,Tangayika
Baadhi ya Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wameiomba halmashauri hiyo kujenga choo cha Kudumu katika Mnada wa Kata ya Mnyagala ambao hukutanisha watu wengi na kusaidia halmashauri hiyo kupata Mapato.
Halima Kitumba kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika akitoa ufafanuzi wa Hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Madiwani katika kikao hicho |
Baadhi ya Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wameiomba halmashauri hiyo kujenga choo cha Kudumu katika Mnada wa Kata ya Mnyagala ambao hukutanisha watu wengi na kusaidia halmashauri hiyo kupata Mapato.
Wakizungumnza katika kikao cha Baraza la madiwani Madiwani hao
wamesema kuwa halmashauri imekuwa ikikusanya Mapato kupitia Mnada huo hivyo ni
wakati sasa wa kuona umuhimu wa Kujenga miundombinu ya Choo katika mnada huo.
Watumishi na wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani |
Pamoja na hayo diwani huyo amasema kuwa kutokana na Msongamano
wa wawatu katika mnada huo kutokuwa na huduma ya choo kunaweza kusabisha
Magojwa ya Mripuko kwa wananchi.
Amina Lubwe Diwani wa Viti maalumu katika Kata ya Mnyagala
amesema kuwa halmashauri imekuwa ikikusanya ushuru katika mnada huo ambao
hufanyika mara mbili kwa mwezi hivyo ni mhimu halmashauri kuchukua jitihada za
haraka kujenga miundo mbinu hiyo ya choo.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika pamoja na wakuu wa idara na watumishi wakiwa katika kikao hicho |
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Halima
Kitumba amesema kuwa halmashauri itafanya kila linalowezekana na kuchukua hatua
za kujenga Miundombinu ya choo katika mnada huo ili wananchi waendelee kufanya
kazi zao vizuri na halmashauri iendelee kupata Mapato.
‘’Niwaahidi watoa hoja ofisi ya Mkurugenzi itakwenda kujenga miundombinu hii kwa haraka iwezekenavyo ili wananchi wapate huduma katika mazingira salama na sisi halmashauri tuendelee kukusanya mapato’’ amesema Kaimu Mkurugenzi huyo Halima Kitumba.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Philmoni Molo [katikati]akiongoza kikao hicho |
‘’Mkurugenzi hamwezi kukushidwa kutafuta fedha ya dhalula
kwaajili ya ujenzi wa matundu mawili ya vyoo kwenye mnada huuamesema ‘’Makamu
mwenyekiti huyo wa Halmshauri hiyo.
Diwani wa Kata ya Tongwe Frank Kibigas amehoji kuwa kuna
kigugumizi gani kwa halamsahuri kutopeleka fedha za miradi katika kijiji cha
Ngoma Lusambo ambapo tangu 2017 kunaboma la zahanati ambalo wananchi
wamejitolea kulijenga.
‘’Mh mweyekiti hivi shida ni nini kutopeleka fedha kwa wananchi hawa wa Kijiji cha Ngoma lusambo wananchi hawa wanapata shida tuwaonee huruma’’ alisema Diwani huyo
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tanganyika Yasin
Kibiriti wakati akitoa neno kwa niaba ya chama katika Baraza hilo amesema
halmashauri nivyema kutafuta fedha ya dhalula ili kuhakikisha miradi ambayo
haijapatiwa fedha ipelekewe fedha.
‘’Sisi kama chama kazi yetu ni kushauri niishauri ofisi ya mkurugenzi kutafuta fedha ya dharula ili miradi iliyolalamikiwa na waheshimiwa madiwani ipelekewe fedha huko ndipo walipo wapiga kura wetu wa CCM’’ amesema kibiriti