MADIWANI MLELE WALIA UMEME KUTOFIKISHWA ILUNDE

 

Makamu Mwenyekiti wa Halamshauri ya Wilaya ya Mlele Alphonce Kiyungi akiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani 

Na Paul Mathias,Mlele.

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamemuomba mkandarasi anaesambaza umeme Vijijini kufikisha  huduma ya umeme katika Kituo cha afya Ilunde ili wananchi wapate huduma kwa wakati.

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani

Baraza la Madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamemuomba mkandarasi anaesambaza umeme Vijijini kufikisha kwa haraka huduma ya umeme katika Kituo cha afya Ilunde ili wananchi wapate huduma kwa wakati.

Madiwani hao wameyabainisha hayo wakati wakichangia taarifa za taasisi katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo.

Diwani wa Kata ya Ilunde Maltin Mgoloka amesema serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan imelefedha na kujengwa kwa Kituo cha Afya Ilunde lakini huduma ya umeme bado haujafika kwenye Kituo hicho.

Watumishi na wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Mlele wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani.

‘’tunaendelea kupoteza wananchi Ilunde serikali ya Dk Samia imetupa fedha  tukajenga kituo kikubwa cha Afya na sasa tunapokea vifaa ikiwemo Jokofu la Damu Salama tunachumba cha upasuaji lakini vyote hivi havifanyi kazi sababu hatuna umeme na juzi kuna mama amefariki dunia kwa ukosefu wa damu lakini umeme ungekuepo asinge poteza maisha mama Yule amesema ‘’Mgoloka

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nsekwa Eligius Malando amesema kuwa kituo cha afya Ilunde kimekamilika kwa muda sasa lakini kukosekana kwa huduma ya umeme ni tatizo kwani kuna vifaa vinahitaji nishati ya umeme ili vifanye kazi.

‘’tuombe sasa umeme huu ufike pale kituo cha afya Ilunde haraka kwani kuna vifaa tiba vinahitaji umeme ili kufanya kazi kuchelewa kufika kwa umeme kuna fanya utoaji wa huduma kutokuwa ya ufanisi’’ amesema Diwani Malando.

Kaimu Meneja wa Shrikala la Umeme Tanesco Wilaya ya Mlele Hussein Mzanva akijibu hoja mbalimbali zinazohusu umeme zilizoibuka kwenye kikao hicho.

Aidha Diwani wa Kata ya Utende Deus Bundala wakati akichangia taarifa ya Shirika la Umeme Tanesco kwenye kikao hicho amesema kuwa Kasi ndogo ya ujenzi wa  Mradi Grid ya Taifa unaenda kwa mwendo wa Kinyonga hali inayopelekea baadhi ya wawaekezaji kushidwa kufanya uwekezaji wa kutosha kutokana na huduma ya umeme kuwa ya kusuasua.

‘’mradi wa Grid ya taifa nimradi mkubwa wenye gharama kubwa lakini katika taarifa hii inaonekana mradi huu utakamilika lakini sioni kama kuna dalili ya kukamilika kwa mradi huu kutoka Tabora hadi hapa mkoa wetu wa Katavi ameeleza ‘’Diwani Bundala

Hussein Mzanva Kaimu meneja wa Shirika la umenme Wilaya ya Mlele amesema hadi kufikia mwezi wa kumi na moja wanatarajia kuwasha umeme katika Kata ya Ilunde na kijiji cha Isegenezya.

Diwani wa Kata ya Utende Deus Bundala akitoa hoja katika kikoa  hicho.

‘’mkandarasi wa Rea katika mkoa wetu yupo mmoja na sasa yupo Tanganyika na ukizingatia umbali wa kutoka Mapili hadi ilunde nimakadilio ya kilomita 45 nimtoe hofu diwani wa Ilunde mpango wetu ni kuwasha umeme kata ya Ilunde na Kijiji ch Isegenezya ifikapo mwezi wa 11 mwaka huu amsema Mzanva.

Kuhusu ujenzi wa Mradi wa umeme Grid ya Taifa kutoka Tabora amesema kuwa katika siku za hivi karibuni kulikuwa na tatizo la kibajeti na fedha ilikuwa inatoka kwa awamu kwaajili ya kuendelea na mradi huo na tayari wameongezewa muda wa miezi nane ili kukamilisha Ujenzi huo.

Baadhi ya Viongozi wa Vijiji na Kata Halmashauri ya Wilaya ya Mlele wakisaini  Sheria ndogo za Vijiji zilizopitishwa na Baraza hilo kutumika katika Vijiji vya Halmashauri hiyo.

’kutokana na matatizo ya kifedha fedha haikutoka kwa wakati hivyo wametuongezea muda wa miezi Nane ambapo tutakwenda hadi mwaka 2024 Mwezi wa Nne ili kukamilisha kuunganisha umeme wa grid ya Taifa  amebainisha Mzanva.

Makamu mwenye Kiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Alphonce Kiyungi akifunga kikao hicho cha baraza la Madiwani ameishukuru serikali kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za miradi ya Maendeleo katika halmashauri 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages