Naibu waziri wa Mali asili na Utalii Mary Masanja akiizindua Rasimi Hotel ya Home Ground iliyopo mkoa wa Katavi. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi
Hifadhi ya Taifa ya
Katavi ambayo ni moja ya Hifadhi tano kubwa hapa nchini
itanufaika na Hoteli Mpya ya Kitalii na yakisasa yenye uwezo
wa vyumba vya kulala viongozi inayoitwa Home Ground ambayoitasaidia
kukuza mtandao wa utalii katika eneo la huduma na malazi kwa
watalii wanaokuja nchini .
Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambayo ni moja ya Hifadhi tano kubwa hapa nchini itanufaika na Hoteli Mpya ya Kitalii na yakisasa yenye uwezo wa vyumba vya kulala viongozi inayoitwa Home Ground ambayoitasaidia kukuza mtandao wa utalii katika eneo la huduma na malazi kwa watalii wanaokuja nchini .
Hoteli hiyo
ya nyota tatu ya kwanza katika Mkoa wa Katavi iliko
katika Mtaa wa Ilembo Manispaa ya Mpanda
imefunguliwa na Naibu Waziri Maliasili na Utalii
Mary Masanja aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo
.
Katika hotuba yake ya
ufunguzi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amesema hoteli hiyo ya
kitalii ya Home Ground kufunguliwa kwake
itasaidia kukuza mtandao wa watalii
wanaokuja nchini kutembelea hifadhi ya Taifa ya Katavi
katika eneo la huduma na malazi .
Amebainisha kuwa uwekezaji wa hoteli hiyo Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambayo ni moja ya hifadhi kati ya hifadhi kubwa tano za hapa nchini ambayo inaukubwa wenye kilometa za mrada 4,471 kuwa na uhakika wa malazi ambayo mtalii yoyote au viongozi wa kiserikali kuweza kupata huduma hapo .
Masanja alisema
kuwa uzinduzi wa hoteli hiyo ni mwendelezo wa ushirikiano wa
Sekta binafusi na Serikali katika utoaji wa huduma za maradhi hapa
nchini na pia linaunga mkono juhudi za dhati
za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kama
alivyoelekeza katika filamu ya The Royal Tour.
Ameipogeza kampuni
ya Home Ground kwa uwekezaji huo mkubwa
walioufanya hali ambayo imefanya kuwepo na ongezeko na
huduma za malazi zikiwa zmeomgezeka katika Mkoa wa Katavi na hapa
nchini .
Amewahakikishia wawekezaji hao na wawekezaji wengine kuwa Serikali itazidi kuweka mazingira mazuri wezeshi ili kudumisha ushirikiano katika kukuza na kuongeza idadi ya watalii wanaofika katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi inayosifika kwa kuwa na wanyama wakubwa kuliko hifadhi nyingine akiwepo na twiga mweupe .
Naibu Waziri
Masanja ameisisitiza bodi ya wakurugenzi wa Hoteli hiyo kuhakikisha
wanatowa huduma zuri kwa wateja kuanzia kwenye mapokezi pindi
mgeni anapokuwa amefika hapo ili waweze kuendelea kupata wageni
zaidi .
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Bodi ya hoteli ya Home Gground
Willy Mbogo alisema kuwa ujenzi wa hoteli hiyo ya kitalii
ilianza kujengwa toka mwaka 2019 na mpaka sasa
imefikia asilimia 95 na imegharimu kiasi cha shilingi
Bilioni 3.5 na ikikamilika sehemu ya ukumbi itakuwa imegharimu
kiasi cha shilingi Bilioni 4.
Amesema hoteli
hiyo inavyumba 38 ambapo katika ya vyumba
hivyo vyumba vitano vinahadhi ya kulala viongozi
wa Kiserikali amewaomba wadau mbalimbali kutowa ushirikiano
kwenye hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano .
Aidha Mbogo ameiomba Serikali kuboresha mazingira ya miundo mbinu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na kuweka mazingira rafiki ya wawekezaji ndani ya hifadhi nan je ya hifadhi ya Taifa ya Katavi .