Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani. |
Na Walter Mguluchuma,
Katavi .
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kuwakamata watoto 45(DAMU CHAFU) ambao wamekuwa wakijihusisha kufanya matendo mbalimbali ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda na kupelekea kuwafanya wananchi wa Manispaa ya Mpanda kuhofia hali ya usalama wao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amewaambia wandishi wa Habari damu chafu hao wamekamatwa kufatia msako mkali ulifanywa na jeshi la Polisi kufatia kuwa kumejitokeza matukio mbalimbali ya uhalifu katika Mji wa Manispaa ya Mpanda .
Alisema jeshi hilo limekamata Damu chao 45
wenye umri wa kuanzia miaka kumi na moja mpaka miaka 17 ambao
waliweza kukamatwa na kushikiliwa na polisi katika watoto hao
waliowakamata waliweza kusaidia jeshi hilo kuweza kuwapata vijana
wengine wahalifu wenye umri kati ya miaka 18 hadi miaka
24.
Amebainisha kuwa vijana hao kumi na nane
waliotajwa na damu chafu kushirikiana nao kufanya vitendo vya
uhalifu wamekiri kujihusisha na vitendo hivyo vya yhalifu kwamba ni kweli
wanafanya vitendo hivyo katika maeneo mbalimbali
yanayozunguka mji wa Mpanda .
Kamanda Ngonyani alieleza kuwa katika hao
vijana kumi na nane waliokamatwa wameweza nao
kuwataja watu wengine ambao bado wanaendelea kusakwa na jeshi
la polisi ambao ni wakubwa na wengine kati yao wakiwa wametoka
gerezani hivi karibuni kwa msahamu
uliotolewa mwezi Aprili mwaka huu.
Kati yao wawili walikuwa wamemaliza vifungo vyao
na mmoja wameweza kumkamata na mmoja ambae amekuwa
akihusika na matukio bado wanaendelea kumtafuta kwani yeye
ndio amekuwa akifanya matukio makubwa makubwa kwani wao damu chafu
wao wamekuwa wakijihusisha na matukio madogo madogo .
Alisema baada ya kukamatwa kwa damu chafu 45
jeshi hilo liliungana na ofisi ya Ustawi wa Jamii
Manispaa ya Mpanda na waliweza kukaa na wazazi wa watoto hao na wailiweza
kuwapeleka Mahakamani na kupewa kibali na Mahakama kwamba watoto hao
watakuwa wanaripoti kituo cha polisi baada ya muda wao wa masomo
kuwa umekwisha saa kumi na mbili jioni kila siku .
Amefafanua kuwa wananchi wa Manispaa ya Mpanda
waondokane na hiyo taaruki ya kudhani matukio yote yanafanywa na damu
chafu matukio makubwa yanafanywa na watu wazimu wao damu chafu ni
watoto wadogo na ndio wamewasaidia kuwapata hao walifu 18 wakubwa
na wameisha wapeleka Mahakamani kwa matukio waliyokuwa wameyafanya .
Na kwa kukamatwa kwa watu hao jeshi la polisi
limewezakufanikiwa kukamata vitu vingi kwa hao wahalifu wenye umri
wa zaidi ya miaka 18 na kuendelea baadhi ya maeneo
waliweza kufa wizi huo wa viti ni kwenye eneo la Mtaa wa Ilembo
na wameweza kuwakabidhi wahusika wa mali hizo walizokuwa wakizipora
kwa kuwakata watu kwa mapanga .