KAMISHNA TAWA SERIKALI KUSHUGHULIKIA MIPAKA YA MAPORI.

 

 

Kamishina Mkuu wa TAWA,Mabula Miswingu Nyanda akizungumza na wafugaji wa nyuki katika wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi

Na George Mwigulu, Nsimbo.

Serikali kupitia Wizara ya maliasili na utalii imeuda kamati maalumu ya  kupitia mipaka ya hifadhi ambapo itawasilisha taarifa ya mipaka ya mapori yote na kutangazwa kwenye gazeti la serikali.


Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe akizungumza na wananchi katika Kata ya Ugalla wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishina Mkuu wa TAWA,Mabula Miswingwi Nyanda.

Amesema hoya jana Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),Mabula Misungwi Nyanda lwakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi ambapo amefanya kikao cha ndani na viongozi wa wilaya pamoja na vikao vya nje na wafugaji nyuki wa Kata ya Nsimbo na Ugalla.

Nyanda alisema kuwa wakati wa kuwekwa kwa alama za mipaka ya mapori,Wananchi watashirikishwa lakini kwa sasa wanapaswa kuzingatia mipaka iliyopo.

Kamishina huyo alisema kuwa mikanganyiko wa mipaka ya uhifadhi za taifa,mapori ya akiba na misitu inatokana na mabadiliko ya kiuhifadhi ambapo baadhi hayakuwepo kwa mfano hifadhi ya taifa ya mto Ugalla kwa sasa hawaruhusu matumizi yoyote ikiwa hapo awali ilikuwa sehemu ya pori la akiba.

 

Kamishina Mkuu wa TAWA,Mabula Miswingu Nyanda akizungumza na wafugaji wa nyuki katika wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi

“ mabadiliko hayo bado serikali inayafanyia kazi kwa ngazi ya wizara kwa sababu TAWA nao hawaanzishi maeneo na kuweka mipaka yao tu.Utaratibu uliopo wa kutenga maeneo kwa upande wa hifadhi wa wanyamapori ni wizara inamamlaka kupitia idara ya wanyamapori hutenga maeneo hayo aidha yawe ya Hifadhi ya Taifa,Pori tengefu au pori la akiba” Amesema Nyanda.

Aidha alisema mkanganyiko wa mipaka unatokana na kuwa hifadhi ya taifa,Pori tengefu na misitu unawafanya wananchi kushindwa kuelewa pori la akiba,misitu na hifadhi ya taifa inaishia wapi na nani anayehusika na taratibu zake zikoje ambapo suala hilo linapaswa kueleweka kwa wananchi kwa ajili ya kuzuia migogoro na kwa kuzingatia hilo amewaelekeza watendaji wa TAWA kutoa elimu?.

 “ wananchi wanatakiwa kuelewa mapori maana yake ni nini  na pori lipi na linahusika na nini na lipi halihusiki na nini hii itawasaidia wakati wananchi wajue wafanyeji na waishije kuendesha maisha yao na kutokufahamu ni sawa na kutembea gizani” Amesisitiza.

 

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Utafiti na Ujirani mwema,Gloria Bideberi akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Ugalla Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi.

Aidha Kamishina huyo alisema kuwa kuna pengo la kutokufahamiana  kati ya watendaji wa TAWA  na wananchi  jambo ambalo linasababisha migongano isiyokuwa ya lazima kwa kuwa na dhana potofu ya kila mtu dhidi ya mwenzake.

Ambapo ametowa wito kwa watendaji wote ya TAWA nchini  kuliondoa pengo hilo kwani wananchi  ni sehemu ya familia zao na majukumu ambayo wamepewa na serikali yasiwatenge bali wanapaswa kuwa na tahadhari na kila kitu kwa ajili ya maisha ya kesho.“kwahiyo mimi na wasihi watendaji wenzagu tuliondoe hili pengo kama ni suala la elimu litolewe” Amesema Kamishina huyo.

Anna Lupembe Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi  amemshukuru Kamishina huyo kwa kusikiliza kero za wafugaji nyuki sambamba kuruhusu kusogezwa huduma ya upatikanaji wa vibali vya kuingia porini ambapo wananchi hulazimika kusafiri umbali wa Km 125 kwenda mji wa Inyonga Wilaya ya Mlele.

Lupembe amesema kuwa suala la wananchi kusafiri umbali mrefu ni kikwazo kwa juhudi za wafugaji nyuki kupiga hatua za maendeleo hivyo uamuzi wa vibali kutolewa katika wilaya ya Mpanda ni wakumkoamboa mfugani hata mdogo wa nyuki.

Baadhi wa Wafugaji wa Nyuki wakito kero zao mbele ya Kamishina Mkuu wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda.

Baadhi ya Wafugaji wa Nyuki wa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wakiwa mejitokeza katika kikao.

Mbunge huyo amesisitiza kuwa wananchi wa Jimbo la Nsimbo hawapendi kufanya uadui na askari wa TAWA kwani kufanya uadui ni kufifisha juhudi za kujikomboa kiuchumi kwao bali wanahitaji kupewa elimu.

Papi Mlela,awali akisoma risala ya mbele ya Kamishina Mkuu wa TAWA watoa ombi kwake kupunguza gharama ya vibali vya kuingia ndani ya pori kwani ni kubwa ambazo wanashinda kuzimudu.

Vilevile wameomba kuruhusiwa kutumia usafiri wa pikipiki kwenda ndani ya pori kubebea asali ambayo wamekwisha kulina kwani itawafanya kubeba kwa wingi zaidi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages