JAMII YAOBWA KUSHIRIKI KUPINGA RUSHWA

 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaibu Kaim[ Kulia] akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majidi Mwanga wakati wa uzinduzi wa Klabu ya Kupinga Rushwa Katika Shule ya Sekondari Kilida


Na Paul Mathias,Mlele

Wananchi na watanzania Kwa ujumla wameaswa kushiriki Kwa vitendo Katika mapambano dhidi ya Rushwa Kwa kutoa taarifa za Rushwa Kwa mamlaka ikiwemo Takukururu Ili serikali kuchukua hatua Kwa watakao bainika kutoa au kupokea Rushwa .

Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Abdalla Shaib Kaim akiwauliza maswali ya ufahamu kuhusu Rushwa wanafunzi wa Sekondari Kilida

Wananchi na watanzania Kwa ujumla wameaswa kushiriki Kwa vitendo Katika mapambano dhidi ya Rushwa Kwa kutoa taarifa za Rushwa Kwa mamlaka ikiwemo Takukururu Ili serikali kuchukua hatua Kwa watakao bainika kutoa au kupokea Rushwa 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaibu Kaim ameyasema hayo wakati akizindua Club ya kupinga Rushwa Katika Shule ya Sekondari Kilida Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoa wa katavi wakati wa Mbio za Mwenge wa uhuru.

Shaibu amesema kuwa Kila Mwananchi anawajibu wa kutoa taarifa za Rushwa Kwa viongozi wake au Katika Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukururu Kwa kupiga simu namba 113 Bure.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akimkabidhi Chandarua mwananchi wa Kijiji cha Songambele Kata ya Kamsisi

''niwaombe Sana wananchi tutoe taarifa za Rushwa bila uoga wowote Kwa viongozi wetu au Katika Taasisi ya Takukuru Ili Sheria na taratibu zichuliwe kwa wale ambao hujihusisha na Rushwa amesema Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa Rushwa ni adui wa haki na kusisitiza wananchi kushiriki na kusimama imara Katika mapambano dhidi ya Rushwa

Aidha amewahakikishia Wananchi kuwa serikali kupitia Takukuru ipo iamara Katika mapambano ya Rushwa Katika Miradi ya maendeleo Ili kuona matokeo ya fedha ambazo hutolewa na serikali Ili wananchi wapate huduma kupitia sekta mbalimbali.

Mwenge wa uhuru Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele umezindua mradi mmoja 1, Umeweka mawe ya Msingi Katika Miradi 3, Pamoja na kuzindua  klabu ya Afya na lishe ya wanafunzi Katika Shule ya Msingi Mgombe na kuzindua klabu ya wapinga Rushwa Katika Shule ya Sekondari Kilida

Shughuli nyingine zilizofanywa na Mwenge wa uhuru kugawa Vyandarua 100 Kwa Wanawake wajawazito na kutembelea shamba la miti la Chama Cha ushirika Cha msingi Ilela Miradi Hiyo ikiwa na Thamani ya Zaidi ya Milioni 653

Mwenge wa uhuru Kwa mwaka 2023 unaenda sambamba na kauli mbiu isemayo TUNZA MAZINGIRA,OKOA NYANZO  VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI KWA UCHUMI WA TAIFA.

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages