WANANCHI MLELE MWENGE WA UHURU UMELETA SULUHU YA MATATIZO.


Mwenge wa Uhuru Mwaka 2023 umezindua zahanati ya kijiji cha Songambele Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ambapo unatarajia kuhudumia watu zaidi ya elfu tano

Na George Mwigulu,Mlele.

BAADHI ya wananchi wa wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi hasa wanawake na wasichana wamepongeza Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023 kwa kuwezesha kuzindua Zahanati,vyumba vya madarasa na uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya kiwango cha lami.

Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,Majid Mwaga akimkabidhi zawadi Mkuu wa wilaya ya Mpanda,Jamila Yusuph baada ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru.

Wakizungumza wananchi hao kwa wakati tofauti leo katika Kjjiji cha Songambele,Kamsisi na Utende wamesema kuwa mbio za mwenge wa uhuru katika wilaya hiyo umekuwa chanzo cha uibuaji wa miradi ya maendeleo.

Jenipher Shigela Mkazi wa kijiji cha Songambele anasema kwa muda mrefu wamekuwa wanaishi na tatizo la kusafiri umbali wa zaidi ya Km 15 kwenda kutafuta matibabu ya afya katika Mji wa Inyonga kutokana na kukosa kituo cha afya au Zahanati ya kuwahudumia iliyo karibu nao.

Jenipha Shigela,Mkazi wa Kijiji cha Songambele Wilaya ya Mlele akizungumzia namna watakavyofaidika na ujenzi wa mradi wa zahanati hiyo.
Elizabeth Lugata,Mkazi wa Kijiji cha Songambele na mama wa watoto sita akielezea namna ambavyo alikuwa anapata adha kubwa ya kusafiri umbali wa km 15 kwenda kutafuta matibabu katika Mji wa Inyonga.

"Kukosa Zahanati kwa muda mrefu ni tatizo ambalo linamkabili hasa mwanamke kutokana na kuwa mama mlezi wa familia anayehakikisha watoto wake wanapata matibabu pindi wanapokuwa wagonjwa.Sasa ndugu Mwandishi huoni hapo mwanamke ndiye anayeathirika zaidi ya baba anayetumia muda mrefu kutokuwepo nyumbani?." Ameuliza Jenipher.

Elizabeth Lugata,Mkazi wa Kijiji cha Songambele anaeleza kuwa changamoto ya kukosa Zahanati ni chanzo cha tatizo la wanawake wengi kujifungulia njiani wakati wakitafuta huduma ya afya na wanawake wengi wameweza kujifungulia majumbani mwao kwa hofu ya kukwepa gharama kubwa ya usafiri na malazi pale wanapokwenda Mji wa Inyonga kutafuta huduma ya afya.

Amesema baada ya Mwenge wa Uhuru kufungua Zahanati ya Kijiji cha Songambele tatizo la kukosa matibabu au kutembea kwa umbali mrefu limekwisha ambapo ameipongeza serikali kwa kuendelea kubuni ujenzi wa mirandi ya maendeleo ambayo lengo lake ni kusogeza huduma kwa wananchi.

Masaja Kadushi,Mkazi wa kijiji cha Utende Wilaya ya Mlele amepongeza mwenge wa uhuru kwa kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa mradi wa barabara ya Uzega- Kafulu ya Km 0.73 ya kiwango cha lami yenye thamani ya zaid ya fedha Mil 379,ambapo amesema kutumia barabara hiyo itarahisishia shughuli ya usafirishaji wa mazao ya chakula na biashara jambo ambalo awali walitapata changamoto ya kushidwa hasa pale mvua zinaponyesha. 

Kadushi,amesema anafahamu mwenge wa uhuru tangu hapo awali akiwa kijana kazi yake ni kumulika maendeleo katika nchi licha ya kuwa mbio zake huambatana na ujumbe maalumu ambao unabeba kusudi kubwa la wananchi kuhimizwa au kupewa tahadhari juu ya jambo fulani.

 

Abdallah Shaib Kaim,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Songambele kwenye uzinduzi wa Zahanati.     

 

 

 

Masaja Kadushi Mkazi wa Kijiji cha Itende akizungumzia masuala ya mwenge wa uhuru.

"Niseme kweli ona sasa hapa umejengwa mradi wa kisasa wa vyumba viwili vya madarasa ya awali shule ya msingi Mgombe,Wilaya ya Mlele kwa ujumla maeneo mengi watoto wetu hawapati shida tena kusafiri umbali mrefu kutafuta masomo kwa kuwa madarasa ya kutosha yapo na sina shaka ufaulu utapanda zaidi" Amesema Kadushi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023,Abdallah Shaib Kaim akiwa katika Zahanati ya Kijiji cha Songambele mara baada ya kufanya ukaguzi na kuzindua zahanati hiyo ameipongeza serikali ya Wilaya ya Mlele kwa kazi nzuri ya kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo kwani amejiridhisha kwamba nyaraka zote za taarifa ya ujenzi wa miradi haina dosari yoyote.

Kaim amesema kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa kusogeza huduma mbalimbali kwa wananchi,serikali itaendelea kutenga fedha nyingi ya miradi ya maendeleo ambapo viongozi wanapaswa kuisimamia ili kuhakikisha thamani halisi ya ubora wa miradi inalingana na fedha zinazotolewa.

Picha hizi zinaonesha vyoo ambavyo vimezingatia wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika shule ya awali  ya msingi Mgombe.


Mahali Bikula,Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Songambele akisoma taarifa mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Abdallah Shaib Kaim katika zahanati ya Kijiji hicho.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Songambele,Mahali Bikula akisoma taarifa ya ujenzi wa Zahanati mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Abdallah Shaib Kaim amesema ujenzi wa Zahanati hiyo ni sehemu ya ujenzi wa Zahanati 6 zilizojengwa mwaka wa fedha wa 2021/22 na 2022/23 ambapo ulianza kutekelezwa mwaka 2022/23 baada ya kupokea fedha Mil 50 kutoka serikali Kuu na baadaye kwa fedha za ndani zaidi ya Mil 64 kwa ajili ya kumaliziaji.

Bikula amesema mradi utagharimu fedha zaidi ya Mil 118 ambapo kukamilika kwake kutapunguza vifo,hasa vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5 sambamba na utahudumia wananchi wanaokadiriwa zaidi ya elfu tano kutoka Kijiji cha Songambele na vitongoji vilivyoko jirani kutoka Vijiji vya Kamalampaka na Kamsisi.

Aidha Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ukiwa katika wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi umezindua/umefungua mradi mmoja utaweka mawe ya msingi katika miradi mitatu,umezindua Klabu ya afya na lishe na wapinga rushwa,kugawa vyandarua 100 kwa wanawake wajawazito na kutembelea shamba la miti ambapo jumla ya fedha zaidi ya Mil 653 zimetumika kwenye miradi

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages