MWENGE WA UHURU WAONYA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.

 


 

 

Abdallah Shaib Kaim,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akizungumza na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Nnsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambapo amehimiza suala la utuzanzaji wa mazingira.


Na Paul Mathias,Nsimbo.

WATANZANIA wameobwa kushiriki vyema Katika utunzaji wa Mazingira Kwa kupanda miti kwenye maeneo yao ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi ambayo yanaonekana Kwa sasa.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Sophia Kumbuli akimkabidhi Mwebge wa Uhuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbi,Mohamed Rammadhani.

Hayo yamebainishwa na kiongozi wa mbioza Mwenge Kitaifa Abdalla Shaibu Kaimu wakati akitoa ujumbe wa Mwenge katika Kijiji Cha Stalike Halmashuri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi.

Shaibu amesema kuwa Kwa sasa Kuna tatizo la Mabadiliko ya Tabia nchi ambayo yamekuwa yakisabisha ukosefu wa Mvua za kutosha kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini Hali ambayo husabisha janga la Njaa Kwa Wananchi.

Katika hatua nyingine amekemea vitendo vya ukataji miti kiholela na uchomaji wa misitu Hali ambayo imekuwa ikiongeza Hali ya ukame na kupotea Kwa uoto wa asili.

Niwaase watanzania wenzangu tujiepushe na ukataji wa miti na uchomaji wa misitu holela.

Kiongozi w Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023,Abdallah ShaIB Kaim (Katikati) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Jamila Yusuph (Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbo Mohammed Rammadhani wakielekea kwenye kukagua mradi wa maendeleo.

 

Moja wa Picha inaonesha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Abdallah Shaib Kaim akishuhudia vipimo vikifanywa na baadhi ya maofisa wa TARURA.

Aidha amewaomba wafugaji kufuga Kwa kuzingatia Sheria Kwa kuheshimu vyanzo vya Maji Ili kuendelea kuwa na maji ya kutosha Kwa matumizi ya kibinadamu.

Ndungu zangu wafugaji tusiharibu vyanzo vya Maji Kwa mifugo yetu tufuge Kisasa Kwa kuwa na mifugo wachache amesema kiongozi huyo wa Mbio za mwenge Kitaifa.

Kuhusu Mapambano ya Rushwa Shaibu ameiomba Jamii Kutoa taarifa ya vitendo vya Rushwa Kwa mamlaka zinazo husika ikiwemo takukururu pamoja na Kutoa ushahidi mahakamani wakati nashauri hayo yakiwa katika vyombo vya utoaji haki.

Pamoja na hayo amewaasa vijana kujiepusha na vitendo vya matumizi ya madawa ya kulevya kwakuwa hupoteza nguvu Kazi ya Vijana wa taifa Kwa miongoni mwao kujihusisha na utumiaji wa Madawa hayo.

Mwenge wa uhuru ukiwavkatika Halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi umezindua na kutembelea miradi Saba Katika sekta ya Elimu,Afya Miundombinu,na mazingira ikiwa na thamani ya shilingi Milioni 898 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages