JENGO LA WAZAZI/UPASUAJI KUPUNGUZA KERO YA WANAWAKE WAJAWAZITO MPIMBWE.


Ni Jengo la Wazazi na Upasuaji ambapo lipo katika Kituo cha Afya Majimoto limewekwa jiwe la msingi na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023,Abdallah Shaib Kaim


Na George Mwigulu,Mpimbwe.

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023, Abdallah Shaib Kaim ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la Mama na Mtoto katika kituo cha afya Majimoto Kijiji cha Ikulwe halmashauri ya Wilaya Mpimbwe Mkoa wa Katavi.

Baadhi ya Majengo ya kisasa yaliyojengwa katika Kituo cha Afya Majimoto halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.

Kukamilika kwa Ujenzi wa Jengo hilo utasaidia kuimarisha utoaji wa huduma ya mama na mtoto katika kituo cha afya Majimoto sambamba na kurahisisha upatikanaji wa huduma ya  za afya kwa wananchi wa Kata ya Majimoto na vijiji vyake.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo Kaimu Mganga MKuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Dkt Martin Lohay kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023 Abdallah Shaib Kaim amesema kuwa mradi huo ulianzishwa na wananchi January 2021 baada ya serikali ya kijiji kutenga eneo la ekari 7.5 zikiwa ni juhudi za kuongeza utoaji wa huduma za afya ambapo hapo awali ni zahanati pekee ya Majimoto ilitoa huduma na kushindwa kukidhi mahitaji kutokana na wingi wa watu wapatao 52,411 kwa mujibu wa sense ya mwaka 2022.

Dkt Lohay amesema kuwa gharama za mradi huo unatokana na makusanyo ya fedha za ndani na jitihada za wananchi ambapo hadi sasa jumla ya fedha zaidi ya Mil 200 zimetumika katika jengo la wazazi na upasuaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Shamim Mwariko akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele,Teresia Irafay yaliyofanyika katika viwanja wa shule ya msingi Ilunda-Mpimbwe. 

Akieleza faida za mradi huo utasaidia kupunguza adha ya wanawake wajawazito,watoto na wananchi wengine kusafiri mwendo mrefu kufuata huduma za afya .

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023, Abdallah Shaib Kaim akiweka jiwe na msingi la Jengo la wazazi na upasuaji amesema kuwa serikali inatumia fedha nyingi kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili kusogeza huduma kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa maendeleo.

Kaim amesema kuwa viongozi wanapaswa kuongeza juhudi za kusimamia miradi hiyo kwa faida ya jamii ambayo ni watumiaji wa huduma mbalimbali.

Moja ya jengo la wangonjwa wa nje (OPD) linalopatikana katika Kituo cha Afya Majimoto halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe.

Baadhi ya vyumba vya madarasa yaliyozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023,Abdallah Shaib Kaim katika halamshauri ya wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi.

Nyanzala Tuma,Mkazi wa Kijiji  Ikulwe amewashukuru viongozi wa halmshauri ya wilaya ya Mpimbwe kwa kazi nzuri ya kuwasogezea kituo cha afya kwani hapo awali wamepata adha kubwa ya kushindwa kupata huduma afya kutoka maeneo ya karibu.

Mkazi hiyo wa Kijiji cha Ikulwe ametoa wito kwa wananchi hasa wanawake kwenda kupata huduma ya afya ya mama na mtoto pindi wanapokuwa wajawazito ili kuweza kuepuka vifo vinavyotokana na kushindwa kuhudhuria katika vituo vya afya.



Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi,Mwenge wa Uhuru umeweza kuzindua jumla ya miradi minne yenye thamani ya zaidi ya fedha Bil 3 ikiwepo uzinduzi wa vyumba vinne vya madarasa  na utengenezaji wa madawati 60 katika shule ya msingi Kilida.

Aidha katika jitihada za kumuuga mkono kauli mbiu ya mwaka huu halmashauri kwa kushirikiana na Asasi za Mazingira wamepanda jumla ya miti 200 ya matunda,imetekeleza kampeni ya upandaji miti kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya nchi  ambapo halmashauri kupitia mradi wa SLR (Urejeshaji Endelevu wa Mazingira) na Hifadhi ya Bioanui Tanzania imeotesha na kupanda miti  7,000 kwenye shamba na ekari 7 zenye thamani ya Mil 4.9

Vilevile  Jumla ya Fedha Mil 31.936 kwa utekelezaji wa agizo la serikali halmashauri ya Mpimbwe imefanikiwa kupanda na kutunza miti 1,500,000 na kugharimu fedha zaidi hizo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages