Na George Mwigulu,Katavi.
MKOA wa Katavi baada ya kutembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023 kwa siku 5 katika halmashauri za wilaya ya Tanganyika,Mpanda,Nsimbo,Mlele na Mpimbwe na kukimbizwa kwa zaidi ya Km 885 umeweza kufikia jumla ya miradi 40 yenye thamani ya fedha zaidi ya Bilioni Tano.
Mwenge huo ukiwa katika halmashauri hizo tano umezindua miradi 22,umeweka mawe ya msingi katika miradi 8 na kukabidhi misaada,kutembelea miradi 10.ambapo baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa barabara za kiwango cha lami,Zahanati na Vituo vya afya,Ujenzi wa miundombinu ya maji safi na salama na upandaji wa miti.
Akizungumza
leo wakati wa makabidhiano kati ya Mkoa wa Katavi na Rukwa ya Mwenge wa Uhuru,Kiongozi
wa Mbio za Mwege wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023,Abdallah Shaib Kaim amesema kuwa usimamizi
bora wa ujenzi wa miradi hiyo unaonesha uimara na mshikamano na uwajibikaji wa
viongozi wa wilaya ya Mkoa.
Kiongozi huyo ameeleza kuwa ujenzi wa miradi hiyo ni kichoche cha ukuaji wa shughuri mbalimbali za uchumi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Mlele,Majid Mwanga akitoa taarifa ya mbio za mwenge wa uhuru zilizofanyika Mkoani hapa. |
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Mlele,Majid Mwanga akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sixtus Mapunda. |
“Tunapongeza Mkuu
wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko kwa kuwa mama bingwa tunaamini kazi kubwa
ambayo tumeiona ndani ya mkoa wake ni kwa sababu ya usimamizi shupavu wa weledi
na umahili wake…tunaomba tufikishie salama zetu” Amesema Kaim.
Aidha,Atupokile
Elia Mhalila Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa ameipongeza serikali ya mkoa wa
Katavi kwa usimamizi bora wa ujenzi wa miradi ya maendeleo kwani wamejenga imani
kubwa kwa rais Samia Suluhu Hassain kwamba hakukosea kuwateua kumsaidia kufanya
kazi.
“Mkoa wa Katavi mmepata Cleansheet kwenye miradi yenu,haikuwa kazi rahisi hata kidogo ndani ya halmashauri tano kufanya vizuri kwenye ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa kufanikiwa kuzinduliwa yote na kuwekewa mawe ya msingi bila hata mradi mmoja kukwama” Amesema Atupokile.
Baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Katavi na wakimbiza mwenge wa uhuru wa Mkoa huo waliohudhuria wakati wa makabidhiano ya mwenge huo kati ya Mkoa wa Katavi na Rukwa. |
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Wilaya ya Mlele,Majid Mwanga akitoa taarifa
kwa niamba ya Mkuu wa Mkoa huo Mwanamvua Mrindoko wakati wa makabidhiano wa Mwenge wa Uhuru katika
kijiji cha Kizi Wilaya Nkasi Mkoani Rukwa amesema wanatambua falsafa ya mwenge wa uhuru ni kuchochea maendeleo,umoja
na amani katika taifa.
Mwaga
amesema Mkoa wa Katavi kwa kuzingatia jitihada za kutekeleza ujumbe wa mbio za
mwenge wa uhuru mwaka 2023 ambao unasema Tunza Mazingira,Okoa Vyanzo vya
Maji kwa ustawi wa viumbe hai kwa uchumi
wa taifa.
Ameeleza kuwa mkoa huo kupitia kupitia Halmashauri za Wilaya ya Tanganyika,Mpanda,Nsimbo,Mlele,Mpimbwe na kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo na uhifadhi wa mazingira wamefanikiwa kupand zaidi ya miche Mil 7 imepandwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa.
Baadhi ya viongozi wa dini kutoka Mkoa wa Katavi waliohudhuria makabidhiano ya mwenge wa uhuru kati ya Mkoa wa Katavi na Rukwa. |
Baadhi ya asikali kutoka Mkoa wa Katavi waliohudhuria wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru kati ya Mkoa wa Katavi na Rukwa, |
Aidha
katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinahifadhiwa,Mkoa wa Katavi umefanikiwa
kutambua jumla ya vyanzo vya maji 102 ikiwamo mito na vijito ambapo serikali ya
Mkoa kupitia halmashauri na wadau wa uhifadhi wa mazingira wamefanya juhudi za
kuvilinda.
Katika
kuhakikisha suala la upandaji miti na utunzaji wa mazingira linakuwa la
kudumu,Mkoa mefanikiwa kuwa na mkakati wa upandaji miti na uhifadhi wa vyanzo
vya maji ili kuweza kufanikisha lengo la kuongeza kasi ya ushiriki wa jamii kwenye upandaji
miti.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa huyo amesema baadhi ya malengo ni kuhifadhi vyanzo vya maji kwa
kushirikiana na jamii,kuzuia uharibifu wa misitu,kuruhusu urejeshwaji wa uoto
kwa njia asili,kuhamasisha upandaji miti na kuhamasisha jamii kwenye utunzaji
na usafi wa mazingira.