Mkuu wa mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi.
Mkoa wa Katavi umewahakikishia
wazazi wa wanafunzi na Wanzania kwa ujumla kuwa wako tayari kuwapokea
wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu kutokana na
kuwa miundombinu ya kutosha ambayo imeisha andaliwa na Mkoa
wa Katavi .
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Mwanamvua Mrindoko wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa
habari jinsi ambavyo Mkoa huu ulivyojipanga kuhakikisha
hakuna changamoto yoyote ambayo inayoweza
kufanya mwanafunzi asiweze kuripoti
shuleni .
Mrindoko amebainisha kuwa wanafunzi
waliofanya mtihani wa kidato cha nne matokeo yake
yameisha patikana na kutangwa mwezi Januari 2023 na
tayari mipango ya kuwapangia kujiunga na kidato cha tano imefanyika
na kwa Mkoa wa Katavi wamepangiwa kupokea wanafunzi 2587 kwa ajiri
ya kujiunga na elimu ya kidato cha tano kwa shule zilipo katika Mkoa wa
Katavi katika shule nane zilizopo katika Mkoa wa Katavi .
Kati ya wanafunzi hao wavulana ni 940 na
wasichana 1,647 na wameanza kuripoti toka tarehe 13
Agosti na mpaka leo Agosti 14
wanafunzi 269 wameisha ripoti shuleni na wanaendelea
kufatila kama Mkoa kuhakikisha wanafunzi wote wanalipori .
Mrindoko amewawahakikishia wazazi
,walezi na wanzania kwa ujumla na wanafunzi kuwa wapo tayari
kuwapokea wanafunzi wote hao kwa kuwa miundo mbinu yoye imekamilika
na ipo ya kutosha kupokea wanafunzi zaidi y ahata
ya hao walichaguliwa .
Ametowa wito kwa wazazi na
walezi wa watoto wanaowalea
ambao wamechaguliwa kujiunga na masomo kwenye shule zote nane zilizopo
katika Mkoa wa Katavi wahakikishe wanafanya utaratibu
utakaowawezesha wale wanafunzi ambao hawajaripoti waweze
kuripoti mapema ili waweze kuungana na wenzao ambao wameanza masomo
.
Mkoa umeisha weka utaratibu mzuri wa walimu wa kuwapokea kwa muda wote wanakuwepo na namba zao za simu zinakuwa wazi ili kuweza kutowa huduma kwa haraka zaidi .