Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani |
Na Walter Mguluchuma,Katavi
Katika hali isiyo
ya kawaida wananchi wa Tarafa ya Karema mwambao
mwa ziwa Tanganyika Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi
wamechangishana fedha kwa ajiri ya kumpeleka mganga wa
kienyeji(Kamchape] ili afike kijijini hapo kuweza kufanya kazi
ya kuwabaini na kuwatambua watu wanao daiwa kuwa ni washirikina(wachawi)
Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wa Tarafa ya Karema mwambao mwa ziwa Tanganyika Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wamechangishana fedha kwa ajiri ya kumpeleka mganga wa kienyeji(Kamchape] ili afike kijijini hapo kuweza kufanya kazi ya kuwabaini na kuwatambua watu wanao daiwa kuwa ni washirikina(wachawi)
Baadhi ya wananchi
hao wamesema kuwa ni kweli wameamua kuchangishana fedha za
kumleta mganga wa kienyeji anaeitwa Kamchape ili aweze
kuwatambua watu ambae wamekuwa wakijihusisha na maswala ya
ushirikina kwenye kijiji cha Karema .
Mmoja wa wakazi wa
Kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Boki amesema
swala hilo kwa hapo kijiji la kuchanga fedha kwa ajiri ya
kumleta kamchape limeungwa mkono na watu wengi wa Kijiji
hicho licha ya kuwa anavyotambua yeye swala hilo
Serikali imeisha piga marufuku .
Amebainisha kuwa
karibu asilimia tisini ya wananchi wa Kijiji cha
Karema husani vijana wanaunga mkono kwa asilimia
mia mganga huyo kamchape afike kijijini hapo ili
aweze kuwabaini watu wote kwenye kijiji cha Karema
ambao wanajihusisha na maswala ya ushirikina .
Nae mkazi mwingine
wa Kijiji hicho ambae hataka jina lake litajwe
alisema wanalazimika kuchanga mchango huo ambao hadi sasa
kuna zaidi ya shilingi laki tano kwani endapo hutaonekana wewe
hutaki kuchangia jamii itakuchukulia kuwa na wewe ni mshirikina
ndio maana unaogopa kamchape asifike kijijini hapo .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Katavi Kaster Ngonyani amesema hapo siku za nyuma watu hao
wanaojiita kamchape wanaodai kuwa wanatambua wachawi walikuwa
kwenye Kata ya Ikola Tarafa ya Karema hata hivyo jeshi
la polisi kwa kushirikiana na jeshi la wananchi waliweza kuwafukuza
kundi hilo la kamchape kabla hawajaanza kufanya kazi yao hiyo .
Kamanda
Ngonyani amewaonya watu hao kutofanya shughuli hiyo
kwani matokeo ya kazi hiyo ni kusababisha mauaji kwa watu wasio na hatia
hivyo watahakikisha wanawazuia kabisa kamchape kufanya
kazi hiyo ambayo haina tofauti na lamli chonganishi
ambayo imekuwa ikikazwa na jeshi hilo kwa nguvu zote.