Na Paul Mathias,Tanganyika
Mwenge wa uhuru katika Wilaya ya Tanganyika
Mkoa wa Katavi imezindua miradi Saba yenye Thamani ya Shilingi Billion 1.5
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Shaib Abdalla Kaim Mwenyekombati Nyekundu [Katikati] akiwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika
Mwenge wa uhuru katika Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi imezindua miradi Saba yenye Thamani ya Shilingi Billion 1.5
Akizungumza Kwa nyakati tofauti akiwa katika uzinduzi wa miradi hiyo katika Wilaya ya Tanganyika kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla shaib kaim amesema ameridhishwa na miradi hiyo.
Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Tanganyika Eng Alkam Sabuni akitoa maelezo ya Mradi wa Maji Vikonge katika mchoro kwa Kiongozi wa Mbioza Mwenge Kitaifa Abdall Shaib Kaim. |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim [Kulia] akiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu[Kushoto] muda mchache baada ya kuzindua Mradi wa Maji Vikonge |
Kiongozi huyo wa mbio hizo za Mwenge amezindua Shule ya awali na MsingiNtikimo iliyotokana na Fedha za Mradi wa Boost ambapo Serikali imeleta zaidi ya Milioni 600 Kwaajili ya kufanikisha ujenzi huo wa Shule.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akiwa katika ukaguzi wa Majengo ya shule ya Awali na MsingiNtikimo Kijiji cha Kasekese kabla ya kuzindua Mradi huo |
Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Sibwesa Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi walijitokeza kuulaki Mwenge wa uhuru ulifika kijijini hapo. |
Mwenge wa uhuru Kwa mwaka 2023 unaenda sambamba na kauli mbiu inayo Sema Tunza Mazingira okoa vyanzo vya Maji Kwa usitawi wa viumbe hai na uchumi wa taifa.