Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Shabani Juma [aliyevaa miwani] akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli [wakwanza kushoto] |
Na Paul Mathias,Mpanda
Mwenge
wa Uhuru katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda umezindua Mradi wa Maji katika
katika Kijiji cha Kakese Uliogharimu kiasi zaidi ya cha Shilingi Milioni 951.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akizindua Mradi wa Maji katika Kijiji cha Kakese. |
Akizindua
Mradi huo kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaibu Kaim amesema kuwa
Mradi huo ni sehemu ya Serikali ya wamu ya Sita ya kumutua mama ndoo kichwani
ili kusogeza Huduma ya maji karibu na makazi yao hususani maeneo ya Vijijini.
Katika
hatua nyingine Kaimu ameipongeza Ruwasa Wilaya ya Mpanda kwa kuu simamaia Mradi
huo mpka kukamilika kwake ili uwanifaishe wananchi.
‘’niwapongeze
sana Ruwasa kwa usimamizi huu tumendembelea mradi tumeona Matenki na eneo hili
vyote vipo salama’’ amesema Shaibu Kaimu Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa alipokuwa
anazindua Mradi huo.
Mbunge
wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi akitoa salamu kwa wananchi katika
uzinduzi wa Mradi huo amesema kuzinduliwa kwa mradi huo wa Maji kakese ni
sehemu ya juhudi za serikali ya kuhakikisha inaendelea kupunguza tatizo la
upatikanaji wa Maji maeneo ya vijijini.
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi akimtua mama ndoo kichwani muda muchache baada ya mradi wa Maji Kakese kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru |
''kupitia Ruwasa Visima vimeendelea kuchibwa nia ya Rais Dk Samia ni kumtua mama ndoo kichwani kupitia uzinduzi huu wa Maji kilio cha maji kwa wananchi wa Kakese umepatiwa ufumbuzi ''amesema Kapufi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila yusuph akielezea miradi itakayo tembelewa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru Katika Wilaya ya Mpanda. |
Mwenge
wa uhuru katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda umekimbizwa Jumla ya Kilomita
92 na kuifikia miradi 11 katika sekta ya Elimu,Afya,Maji na Miundombinu huku
Miradi 6 ikizinduliwa na Miradi miwili ikiwekewa Jiwe la Msingi na mingine
Miwili ikitembelewa miradi hiyo inajumla ya Shilingi Bilioni 1.7
Mwenge wa uhuru Kwa mwaka 2023 unaenda sambamba na kauli mbiu inayo Sema TUNZA MAZINGIRA OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USITAWI WA VIUMBE HAI NA UCHUMI WA TAIFA.