Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi,Faustine Maijo. |
Na Walter Mguluchuma, Katavi.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imewaonya watu wanaojifanya watapeli watu wanaowapigia watu simu na kujitambulisha kwao kuwa wao ni maafisa wa Takukuru waache tabia hiyo mara moja kabla hawajatiwa nguvuni .
Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa TAKUKURU
Mkoa wa Katavi Faustine Maijo wakati alipokuwa akitowa
taarifa ya utekelezaji wa kazi katika kipindi cha miezi mitatu ya
kuanzia Aprili hadi June 2023.
Amebanisha kuwa bado kumekuwepo na wimbi
linalioendelea la watu matapeli wanaojifanya
ni maafisa wa Takukuru ambao huwapigia watu simu kwa lengo la
kuwatapeli kuwa wao ni maafisa wa Takukuru na kuwataka waweze
kuonana nao kwa madai wao ni wahusika wa Taasisi hiyo ,
Maijo amewaonya matapeli kuacha tabia
hiyo mara moja kwani watambue kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai
na watakao thubutu kujifanya maafisa wa
Taasisi hiyo watambue kuwa watakamatwa mara moja kwani
wameisha jipanga kukomesha kabisa katika Mkoa wa
Katavi wimbi hilo .
Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa wa Katavi
ametowa wito na rai kwa jamii na watumishi wa Mkoa wa
Katavi ambao ikitokea wamepigiwa simu na matapeli hao
watowe taarifa kwenye osifi ya Takukuru iliyokaribu nae
kwa kupiga simu namba 113.
Amewataka watu wasikubali kutapeliwa na watu hao
bali watowe taarifa mapema Takukuru ili
mhalifu au wahalifu aweze kuchukuliwa hatua za kisheria
mapema kwani ni kosa la kisheria kujifanya
mtumishi wa TAKUKURU .
Adha alisema Takukuru Mkoa wa Katavi
wameendelea na utekelezaji wa majukumu yake
katika robo mwaka kwa kipindi cha mwezi A
prili hadi June 2023 mkazo uliwekwa katika elimu
ya kuhamasisha wananchi ili washiriki kikamilifu
kuzuia rushwa na ufatiliaji wa fedha za miradi ya
maendeleo zilizotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na
kufanyia kazi maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na viongozi
wa nchi .