TAKUKURU KATAVI IMECHUNGUZA FEDHA BILIONI 2.8 ZILIZOINGIZWA.

 

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi Faustine Maijo akizungumza na wanahabari leo katika ofisi za Taasisi hiyo.


Na Walter Mguluchuma, Katavi.

Taasisi ya Kuzuia  na  Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa  Katavi  katika  kipindi cha miezi  mitatu  imefatilia  utekelezaji  wa Miradi  yenye thamani ya zaidi ya  shilingi Bilioni  2.8 katika kipindi cha miezi mitatu kwenye  sekta za  Barabara , elimu  na  Afya.

Hayo amesema  Mkuu wa  Faustine  Maijo wakati aliokuwa akitowa taarifa  ya utekelezaji kazi wa  Taasisi  hiyo  kwa kipindi cha  miezi mitatu ya kuanzia  mwezi  Aprili  hadi June  ambapo  sehemu  kubwa walimejikita katika   kushughulikia  wazabuni  waliosababisha  kuchelewa  ukamilishaji wa miradi ya Maendeleo kwenye Mkoa huu.

Amesema  Takukuru  Mkoa wa  Katavi  katika kipindi hicho cha miezi mitatu  imefatilia  utekelezaji  wa miradi  11 yenye thamani  ya shilingi Bilioni  2,831,493,083 katika sekta  za  barabara ,elimu  na  afya .

Maijo  amebainisha kuwa kati ya miradi   miwili  mradi mmoja  unaendelea  vizuri  na miradi nane  inaendelea kufatiliwa  kwa  ukaribu  kutokana na  mapangufu  mbalimbali  ikiwemo  ucheleweshaji  na ubora  wa miradi hiyo

Aidha wameweza  kufanya   chambuzi  za  mifumo  ikiwa lengo    la kutaka kubaini  mianya  ya  Rushwa  ambayoinaweza   kupelekea  vitendo vya Rushwa  kutokea  na  kutowa ushauri  kwa taasisi husika namna  bora ya kurekebisha  mapungufu  yaliyobainika kwenye chambuzi hizo .

Amebainisha kuwa  kwa kipindi  cha  Aprili   hadi june  2023 Takukuru  Mkoa wa Katavi    imefanya  chambuzi  saba  za  mifumo  kwenye  sekta  mbalimbali  ikiwa  ni  pamoja na  ulinzi , vipimo  mistu , maji , maji   miradi ya maendeleo  masoko  na mazingira  katika Halmashauri  za  Mpanda ,Mlele  na  Tanganyika .

Kuhusu uchunguzi wa mashitaka   Takukuru  Mkoa wa Katavi  wameendelea kupokea  malalamiko  yanayohusiana  na vitendo  vya   Rushwa   ambapo  wameweza  kupokea  malalamiko  62 kati ya  malalamiko hayo  taarifa  za Rushwa  ni  45  na  zisizo za  Rushwa ni 17.

Maijo  amesema  katika kipindi cha  Julai   hadi   Septemba  2023 wataendelea kufatilia kwa karibu  frdha zote   zinazotolewa na  Serikali  ili kuhakikisha zinatumika  kama ambavyo  ilivyokusudiwa  na upande  wa miradi  kuwa  na ubora kama  thamani ya  fedha  zinazolingana na thamani ya  mradi.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages