Mkuu wa Wilaya ya Mlele - ALHAJ.MAJID MWANGA akiongea na wajumbe wa kamati ya Afya ya Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Kwenye ukumbi wa mikutano Jengo la utawala Halmashauri ya WILAYA |
Na Kibada Ernest-MLELE
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Alhaj Majid Mwanga amewaagiza Wenyeviti wote wa Vitongoji,na watendaji wa Vijiji kufanya mikutano ya hamasa kuhamasisha wananchi ili waweze kuwa na uelewa pamoja na watoa ushirikiano wa karibu wakati wa zoezi la kutoa chanjo ya polio litakalofanyika tarehe 21 hadi 24 mwezi Septemba mwaka 2023 kwa Mkoa wa Katavi na mikoa mingine hapa nchini
![]() |
Wajumbe wa kamati ya Afya ya Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Mlele wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Mlele Kwenye kikao hicho. |
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Alhaj Majid Mwanga amewaagiza Wenyeviti wote wa Vitongoji,na watendaji wa Vijiji kufanya mikutano ya hamasa kuhamasisha wananchi ili waweze kuwa na uelewa pamoja na watoa ushirikiano wa karibu wakati wa zoezi la kutoa chanjo ya polio litakalofanyika tarehe 21 hadi 24 mwezi Septemba mwaka 2023 kwa Mkoa wa Katavi na mikoa mingine hapa nchini
Mwanga ametoa
maelekezo hayo wakati akifungua kikao cha Kamati ya Afya Msingi cha Wilaya ya
Mlele kilichoketi kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mlele leo
Aidha Alhaji Mwanga ametoa
ombi kwa Viongozi wa dini kuwa siku za Ibada na baada ya
kukamilika Ibada hiyo kwa madhehebu yote kuwatangazia waumini wao
kuwa tarehe ya chanjo ya polio kuwa itakuwa siku ya Alhamisi
tarehe 21-24 mwezi Septemba kuwa itakuwa ni siku ya chanjo,na walengwa
ambao ni watoto wenye umri chini ya miaka minane 8 na kuendelea, hivyo
waweze watu watoe ushirikiano wa kutosha, ili tuvuka lengo tulilojiwekea.
Amesisitiza kuwa
Viongozi wa kisiasa watoe ushirikiano wa kutosha kwa
kushiriki nasi ili tuwe na uelewa wa pamoja ,viongozi waendelee kutoa
hamasa kwa jamii ili wote wawe na uelewa wa pamoja kuhusu chanjo ya polio.
![]() |
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii Bahati Mwailafu akiwa hutubia wajumbe kikao cha Kamati ya Afya Msingi Halmashauri ya Wialaya ya Mlele. |
Mwakilishi wa Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii Bahati Mwailafu ameipongeza timu ya
Uendeshaji wa huduma za Afya ngazi ya Wilaya (CHMT} ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi kwa maandalizi na hatua za haraka zilizochukuliwa baada ya kisa kimoja
cha polio kuripotiwa hapo mei 26 mwaka huu.
Mwakilishi huyo wa
wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Mwailafu amesisitiza kuwa watoto wote
waliolengwa wapatiwe chanjo ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa
Polio,ugonjwa huo ambao unaathiri watoto chini ya miaka 05 hadi 15,
ambapo watoto wote wenye umri chini ya miaka 8 watapatiwa chanjo ya polio.
Kwa upande wake
Mwakilishi wa TAMISEMI Monica Julias amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa
moyo wa upendo na kujituma hasa kwa wahudumu wa afya wawe na moyo wa kuwapenda
wagonjwa maana mapokezi wakati wakija kuoata uhuduma tiba inawafanya wagonjwa
wajione wamepona kutokana na mapekezi jinsi wanavyokirimiwa kwa maneno mazuri
ya kutia moyo na kufariji
Teresia Irafay ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya alishukuru kwa yote yaliyoelezwa
na kuahidi kuwa maelekezo yote yaliyotolewa wataenda kuyafanya kazi.
![]() |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Soud Mbogo akitoa neno kwenye kikao hicho |
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Dkt Thadeus Makwanda ameeleza kuwa lengo la halmashauri ya Wilaya ni kuwapatia chanjo ya polio watoto wapatao 13,658 katika vijiji vyote 18 vilivyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Mratibu wa Chanjo
Halmashauri ya wilaya ya Mlele Haldy Lushats akiwasilisha majukumu ya
Kmati ya Afya ya Msingi ya Wilaya ameeleza kuwa ni kutoa elimu kwa Jamii.kutoa
Taarifa ya Utekelezaji wa chanjo, kumsaidia Mganga Mkuu wa Mkoa na Wilaya namna
ya kutekeleza chanjo,kwa mantiki hiyo kamati ya Afya ya ngazi ya wilaya ipo kwa
mjibu wa sheria na ipo kusaidia upotoshaji wa baadhi ya watu kuwa chanjo zina
madhara.
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Teresia Irafay akielezea namana Halmashauri hiyo ilivyojipanga kutoa chanjo ya Polio kwa watoto kwenye halmashauri hiyo |
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlele Mhe.Soud Mbogo amewasisitiza kutoa ushirikiano kuhakikisha zoezi la chanjo ya polio linafanikiwa kwa halmashauri yote ya Mlele akawataka waendelee kuelimisha jamii kuhakiksha watoto wote lengwa wanapatiwa chanjo.
“Twende
tukahamasishane huko majumbani kwetu ili kufanikisha zoezi hili la chanjo ya
polio kila mtoto anayesitali aweze kupata chanjo ya polio.”amesema Mbogo .