![]() |
Mkuu wa mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizumgumnza na Wananchi wa Manispaa ya Mpanda Eneo la Mpanda Hoteli |
Na Jackson Gerald,Katavi
Serikali katika Mkoa wa Katavi
imeliomba Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Katavi kuwalipa fidia
Wananchi waliopisha Maeneo yao kwaajili ya Kupisha Mradi wa Umeme wa Grid ya
Taifa Katika Mkoa wa Katavi.
Serikali katika Mkoa wa Katavi imeliomba Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Katavi kuwalipa fidia Wananchi waliopisha Maeneo yao kwaajili ya Kupisha Mradi wa Umeme wa Grid ya Taifa Katika Mkoa wa Katavi.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko wakati akizungumnza na wananchi wa Mkoa wa
Katavi Eneo la Mpanda Hotel wakati akisikiliza na kutatua Kero za wananchi
kupitia Mkutano wa Hadhara.
Mrindoko amesema kuwa zoezi la
kuwalipawa Fidia wananchi hao nilamuhimu kwakwuwa wananchi hao wameonyesha
uzalendo kwa kupisha maeneo yao ili mradi huo uweze kufika katika Mkoa wa
Katavi.
‘’kuna baadhi ya wananchi
walibomolewa nyumba zao na miongoni mwao kutofanya uendelezaji wa maeneo hayo
kwa kupisha mradi huo Tanesco fatilieni Malipo hayo ili wananchi hawa wapate
haki yao ‘’amesema Mrindoko.
Hatua hiyo inakuja baada ya
Mwananchi Mmoja aliejulikana kwa Jina la Athumani Jummanne Mkazi wa Mpanda
hotel kupata kufahamu kuwa changamoto ya kutokulipwa kwa Wakati inasabishwa na
nini kwakuwa walibomolewa nyumba zao na kupelekea kuishi kwenye Nyumba za
Kupanga.
‘’Mkuu wa mkoa mimi ni mwaka
mmoja umepita sina sehemu ya kukaa nipo kwenye nyumba za kupanga naomba msaada
wako mimi ninawatoto 6 na wake wawili niwaweka wapi ‘’amesema Jummanne
Kutokana na Changamoto hiyo
Meneja wa Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Katavi Mhandisi Seraphine
Lyimo amekili kuwepo kwa changamoto hiyo nakubainisha kuwa kulikuwa na
changamoto ya kimfumo wa Malipo na kuwaomba wananchi hao kufika ofisi za
Tanesco mkoa ili kuhakiki majina yao na taratibu zingine kuendelea.
‘’Malipo ya fidia kwa wananchi waliopitiwa na Mradi wa Umeme wa Grid ya Taifa tayari yameshafanyika kwa baadhi ya Wananchi katika Wilaya za Mkoa wa Katavi ingawa kuna baadhi yao hawajalipwa kutokana na mchakato wa kufanya Tathimini ya Mali zilizopitiwa na Mradi huo amesema Lylimo.