HALMASHAURI YA NSIMBO YAJIWEKEA MIKAKATI KUPUNGUZA UDUMAVU

 

Baadhi ya watoa huduma Ngazi ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakiwa katika kikao cha Robo ya mwaka chenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu Masuala ya Lishe Pamoja na uzazi salama

Na Paul Mathias,Nsimbo

Watoa huduma za afya Ngazi ya Jamii katika halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi wamepomgeza mkakati wa Serikali kwa kushirikiana halimashauri kuwapa elimu juu yanamna bora ya kutekeleza afua za lishe kwenye maeneo yao hali ambayo itasaidia kupunguza Hali ya Udumavu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mohamed Ramadhani akizungumnza na Mwandishi wa Habari wa Chombo hiki kuhusu namna halmashauri ilivyojiwekea Mikakati ya Kutokomeza Udumavu.

Watoa huduma za afya Ngazi ya Jamii katika halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi wamepomgeza mkakati wa Serikali kwa kushirikiana halimashauri kuwapa elimu juu yanamna bora ya kutekeleza afua za lishe kwenye maeneo yao hali ambayo itasaidia kupunguza Hali ya Udumavu.

Wakizungunza kando ya kikao kazi kilichofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo watoa huduma ngazi ya Jamii wamesema kuwa kupitia mafunzo mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa na wataalamu wa Masuala ya lishe kwenye Halamsahuri ya Nsimbo imesaidia pakubwa  kutoa elimu ya lishe maeneo ya Vijijini.

Profili Ngunga Mtoa huduma za afya ngazi ya Jamii kutoka kijiji cha Isanja Ndugu Kata ya Nsimbo anasema kuwa amekuwa akifikisha ujumbe kuhusu Masuala ya Lishe kwa kuzitembelea kaya ili kuhamasisha umuhimu wa kuzingatia lishe bora.

Watoa huduma Ngazi ya Jamii Halmashauri ya Nsimbo wakiwa katika kikao kazi kwaajili ya kusaidia jamii kuhusu Masuala ya Lishe

’'Tunawaelimisha vizuri sana wanapokea tunacho waeleza na wengine wanatoa ushuhuda kwetu kweli hiki mnacho tufundisha kimetusaidia sana kufahamu makundi ya vyakula’’ anasema Ngunga

Niyongele Masabe Mtoa huduma za afya ngazi ya Jamii kutoka Kijiji cha Ndui Station kata ya Katumba amesema kuwa tangu mpango huo unazishwe kumekuwa na Mabadiliko kwa wanajamii kutoka maeneo wanayotoka kutokana na elimu wanayoitoa kwa wakazi hao kuhusu lishe na masuala ya uzazi salama.

‘’Kwakeli akina baba akina mama wameanza kubadilika tukiwa kwenye kituo cha afya Katumba tunatoa elimu akina mama wanaelewa kwenye masuala ya uzazi pamoja na mambo mhinu ya kuzingatia wakiwa katika hali ya ujauzito ili kumlinda mtoto alieko tumboni tunashuru wanatuelewa ‘’anasema Niyongele

Jackline Kitomali Afisa lishe Halmashauri ya Nsimbo amebainisha kuwa kupitia watoa huduma ngazi ya Jamii wamekuwa mabalozi wazuri kwenye maeneo yao kwakutoa elimu ambayo hupatiwa na watalaamu wa masuala ya lishe na uzazi salama.

Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mohamed Ramadhani amesema kuwa halamshauri ya Nsimbo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha udumavu unapungua kwa kuanzisha watoa huduma ngazi ya jamii ikiwa ni  sehemu ya kukabiliana na tatizo la Udumavu ambalo lipo kwa Asilimia 32. Kwenye halmashauri hiyo

‘’Katika Halmashauri ya Nsimbo tumeanza kutoa Elimu kupitia watoa huduma ngazi za Jamii kila robo tunakuwa na Vikao vya ngazi ya jamii kwa lengo la kuwafundisha umuhimu wa Makundi Matano ya Vyakula kwa vitendo kwa usimamizi wa Maafisa watendaji huko Vijijini’’anasema mkurugenzi huyo

Jackline Kitomali Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo akitoa elimu kwa watoa Huduma ngazi ya Jamii kwenye kikao hicho.

Katika hatua nyingine Mohamed ameeleza kuwa tayari wameanza utekelezaji wa upandaji wa Miti ya Matunda katika maeneo ya Taasisi za serikali ikiwemo shule za Msimgi na Sekondari kuhakikisha Miti ya Matunda inapadwa kwa wingi ili kuendelea kupunguzac tatizo la udumavu kwenye Halmashauri pamoja na kilimo cha Mbogamboga katika ngazi ya Kaya.

Katika kukabiliana na tatizo la Udumavu Niwajibu kuzingatia Makundi Matano ya Vyakula ikiwemo Nyakula vya nafaka Mizizi na Ndizi,Vyakula Jamii ya Kunde na vyenye asilia ya Wanyama,Matunda,Vyakula vya Mbogamboga,pamoja na vyakula vya Mafuta,Sukari na Aasali. 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages