WANANCHI WAIBUA MRADI WA BARABARA TARURA YAWAPIGA JEKI

Barabara ya Ilangu Busondo ikiwa katika muonekano 


Na Paul Mathias,Tanganyika.

Wananchi katika Kata ya Ilangu Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wameipomgeza Serikali kupitia Viongozi wa Kata pamoja na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini Tarula Wilaya ya Tanganyika kwa kuanza kuifungua Barabara ya Ilangu Busondo kwa Kiwango cha Changalawe ili kuchochea ukuaji wa Uchumi kwa wananchi hao.

Diwani wa Kata ya Ilangu Sadiki Agustino alipotembelea Barabara hiyo ambayo inaendelea kutengenezwa

Wananchi katika Kata ya Ilangu Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wameipomgeza Serikali kupitia Viongozi wa Kata pamoja na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini Tarula Wilaya ya Tanganyika kwa kuanza kuifungua Barabara ya Ilangu Busondo kwa Kiwango cha Changalawe ili kuchochea ukuaji wa Uchumi kwa wananchi hao.

Wananchi hao wamebainisha hayo wakati wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu kuanza kufanyiwa Matengenezo barabara hiyo yenye urefu wa Km 31 ambayo itaunganisha Kata hiyo na Wilaya ya Uvinza.

Mradi huo uliiibuliwa na wananchi wa Kata hiyo Mwaka 2018 kwa Kwa kushirikiana na Diwani wa Kata hiyo Sadiki Agustino kujitolea kusafisha eneo hilo la barabara kwa lengo kufanikisha shughuli za uchukuzi kwa wananchi hao.

Elias Mbazomtima mkazi wa Kijiji cha Ilangu ‘’anasema tulianza uibuaji wa Brabara ya Ilangu Busondo 2018 chini ya usimamizi wa Mh Diwani Sadiki Agustino aliweza kuhamasisha Wananchi akawaonesha umuhimu wa kufunguliwa hiyo barabara na wananchi waliitikia vizuri na kuungana kwa pamoja kuanza kufyeka na kusafisha eneo hilo la Mradi wa Barabara’’

Mbazo mtima ameishukuru Serikali kwa kuanza Matengenezo kwa kiwango cha Kifusi ikiwa ni ishara ya kuifungua barabara hiyo ambayo wananchi wa Kata ya Ilangu wanaihitaji kwaajili ya shughuli za kiuchumi.

Amina Joel Mkazi wa Kijiji cha Ilangu amesema kuwa ili kuwa inawalazimu kuzunguka KM 68 Kufika uvinza lakini kuanza kufunguliwa kwa Barabara hiyo watatumia Muda mfupi kufika uvinza ambapo ni Jirani kutoka eneo hilo.

Diwani wa Kata ya Ilangu Sadiki Agustino ameeleza kuwa Mwaka 2018 kwa kushirikiana na wanachi walianza kwa Pamoja kuibua mradi huo kwa kufyeka na kusafisha huku wakiwa na imani ya kwamba Serikali itaona jitihada zao.


’'tulifanya utafiti  mdogo sisi kama viongozi wa Kata na baadae tulililileta suala hilo katika vikao vyetu vya kata tukakubaliana kuanza kusafisha pamoja na wananchi nashukuru wananchi walikuwa wanajitolea kwa Makundi’’ anasema Diwani Sadiki

Katika hatua nyingine diwani huyo ameishukuru serikali kupitia Wakala wa barabara za Mjini na vijijini Tarura Wilaya ya Tanganyika kuanza kuitengeneza Brabara hiyo kwa Kiwango cha Kifusi.

‘’Mwaka jana serikali ilileta Shilingi Milioni 90  za kufungua Kilomita 9 na mwaka huu wamepatiwa shilingi milioni 200 kwaajili ya kumalizia ufunguzi wa barabara hiyo ya Ilangu Busondo ambapo Wakandarasi wanaendelea na kazi kwa usimamizi wa Tarura anasema Diwani Sadiki Agustino.

Meneja wakala wa barabara za Mjini na Vijijini Tarura wilaya ya Tanganyika Mhandisi Noalsco Kamasha amesema kuwa hadi sasa wamepokea Kiasi cha shilingi miloni 400 na tayari wapo katika mchakato wa kuanza kutengeneza Madaraja na Makalavati  kwa Mwaka huu wa fedha.

Amesema kuwa barabara hiyo imeanza kufunguliwa mwaka jana na mwaka huu wameanza kumalizia kufungua barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 31.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages