Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Mwalimu Upendo Rweyemamu akifunga Mafunzo ya Siku Nne kwa Walimu 50 wa Somo la Hesabu katika shule za Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Mlele |
Na Paul Mathias,Mlele
Walimu wa Masomo ya Hesabu
katika shule za Msingi Halmashauri ya Wilaya Mlele mkoa wa Katavi wameobwa
kwenda kutumia ujuzi walioupata katika mafunzo maalumu kuhusu Somo la Hesabu Kupitia
Mradi wa Shule Bora unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na
Serikali ya Uingreza kupitia Shirika la UK aid.
Walimu wa Shule za Msingi Mlele wa Masomo ya Hesabu wakiwa katika Majadiliano ya vikundi katika semina hiyo. |
Akifunga mafunzo hayo ya Siku
nne Kwa Walimu hao Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Mwalimu Upendo Rweyemamu amesema
kuwa ujuzi walioupata walimu hao kwa kipindi cha Siku nne ukatumike katika
kuongeza ufaulu wa Somo la Hesabu ikiwa ni Msingi kwa somo hilo katika Masomo
ya Sayansi.
‘’Mafunzo haya mliyoyapata
yanalengo la kuwaongezea umahiri ninyi Walimu wa Hisabati katika kuchanganua
Dhana Mbalimbali za kihisabati tumekuwa tukipata changamoto sababu ya kukosa
Msingi mzuri kwenye Hesabu huku chini watoto hawa wanapanda huku wakijua Hesabu
ni Ngumu Kupitia Mafunzo haya nendeni mkabadilishe Taswila hiyo kwa wanafunzi
wetu’’amesema Rweyemamu
‘’Umahili mliojengewa leo
unakwenda kufanya kitu cha tofauti kwenye Halmashauri yetu na ninyi mnaenda
kuwa Chachu ya Mageuzi na Mabadiliko katika somo hili la Hisabati ukiangalia
katika Takwimu za kitaifa bado Somo la Hisabati halifanyi Vizuri sana wanafunzi
wetu wamekalili Somo hili ni gumu hapana ila ni namna ya wewe mwalimu
unavyomwandaa Mwanafunzi kuhusu somo hilo ukimwambia Somo ni gumu ataendelea
kuamini Somo la Hisabati ni gumu’’ amesema Rweyemamu
Awali akitoa taarifa juu ya
Mradi wa Shule Bora Katika Mkoa wa Katavi Mratibu wa Mradi wa Shule Bora Mkoa
wa Katavi George Mtawa amesema kuwa Mradi wa Shule bora unaofadhiliwa na
serikali ya Uingereza Kupitia Shirika la UK aid kwa kushrikiana na serikali ya
Tanzania katika mkoa wa Katavi wameweza kufanya Mafunzo kwa walimu katika
Halmshauri zote za Mkoa wa Katavi.
‘’Mwezi wa nane tulikuwa na
mafunzo ya Elimu Jumuishi katika Halmashauri ya Mpibwe na sasa hivi tunamafunzo
hapa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kwaajili ya uboreshaji wa ufundishaji wa
Somo la Hisabati kwa Walimu Hamsini kutoka kwenye Shule 25 ambapo kila shule
imeleta walimu wawili ‘’anasema Mtawa
Walimu wa Shule za Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Mlele wanaofundisha Masomo ya Hesabu wakiwa katika Mafunzo juu ya namna bora ya kuongeza ufaulu wa Somo la hesabu |