Na Walter Mguluchuma.Katavi
.
KATIKA hali isiyo ya kawaida idadi ya wanawake walikuwa wanaishi na waume zao katika Kata za Ikola na Karema mwambao mwa Ziwa Tanganyika Wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi wamebakia kuishi bila waume zao kwa sasa kufatia wame zao kuwakimbia kwa kuhofia kukamatwa na Polisi kutokana na tuhuma z a kumuunga mkono mtu anaedaiwa kuwa na uwezo wa kuagua na kufichua wachawi (Kamchape)
Mmoja wa wanawake wa Kijiji cha Ikola
jina tunalo alisema kwa karibu wiki mbili sasa anaishi
bila mwenza wake ambae amemkimbia bila hata ya kumuaga na
kumwachia familia ya watoto watano kutoka na kuhofia kukamatwa na
jeshi la polisi kwa tuhuma za kujiusisha na kundi lilikuwa linamuunga
mkono mganga wa kienyeji (kamchape ) aliyekuwa anadai anao uwezo wa
kubaini washirikina(wachawi)
Amebainisha kuwa Kamchape alipokuwa amefika kwenye Kijiji chao cha Ikola mume wake alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanamuunga mkono Kamchape afanye kazi ya kuwabaini wachawi lakini mume wake alivyoona watu waliokuwa wanamuunga mkono mganga huyo kuanza kukamatwa na Polisi nae pia alitokemea pasipo kujulikana na wala hata mawasiliano nae kama familia hawana
Nae mama mwingine
wa Kata ya Karema ambae hakuta jina lake litajwe
alisema mume wake amekimbia nyumbani kwa kwa muda wa siku kumi sasa
kwa kuhofia kamata kamata inayoendelea ya watu walikuwa
wakiumuunga mkono Kamchape na kufanya uhalifu wa mali mbali
mbali za watu .
Alieleza mume wake aliwaaga nyumbani siku kumi zilizopita
kuwa anakwenda kwenye shughuli zake za kila
siku za uvuvi wa kati akiwa ziwa alipata taarifa za kuwepo kwa msako wa
watu waliojihusisha na uhalibifu wa mali za wafanya biashara wakati wa
Kamchape .
Alieleza kuwa walioathirika na kukumbiwa na waume
zao ni wanawake wengi tuu kwenye maeneo ya Kata ya Karema na pia wapo
baadhi ya wanaume nao wamebaki bila wake zao kufatia wanawake kukimbia
kukamatwa kwan kujihusisha na kumuunga mkono mganga huyo wa
kienyeji .
Nae Mkazi wa Kijiji cha Ikola Emanual Kibiriti
alisema upatikana wa samaki katika maeneo ya Kata
za Ikola na Karema umekuwa ni washida kutokana na wavuvi wengi
ambao ndio walikuwa wakimuunga mkono Kamchape kukimbia na kuacha
kufanya shyghuli yao ya uvuvi .
Amefafanua kuwa idadi kubwa ya wanawake walikimbiwa na
waume zao kutoroka kwa kuhofia kukamatwa na jeshi la polisi ni wake wa
wavuvi wa samaki ingawa pia wapo na wanaume nao wamekimbiwa na wake zao
na kuwaachia watoto.