KILIO MALIPO WAKULIMA WA TUMBAKU KATAVI CHA SIKILIZWA

 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko [wapili kulia] aliposhiriki zoezi la uzinduzi wa Masoko ya Tumbaku Mwezi wa Tano Mwaka huu Katika chama cha Nsimbo AMCOS

Na Walter Mguluchuma,Katavi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia wakulima wa  zao la Tumbaku   katika msimu wa kilimo 2022/2023 ambao  hawaja lipwa   fedha zao zaidi ya Dola Milioni 2.5 kwenye Amcos 6 zilizoingia Mkataba wa ununuzi wa Tumbaku na Kampuni ya Mkwawa Leaf LTD  zinatarajiwa kulipwa hivi karibuni na  kampuni hiyo.  

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akisaini mfano wa Bello Tiketi ya Tumbaku wakati wa uzinduzi wa Masoko ya Tumbaku mkoa wa Katavi mnamo Mwezi May Mwakaa huu

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia wakulima wa  zao la Tumbaku   katika msimu wa kilimo 2022/2023 ambao  hawaja lipwa   fedha zao zaidi ya Dola Milioni 2.5 kwenye Amcos 6 zilizoingia Mkataba wa ununuzi wa Tumbaku na Kampuni ya Mkwawa Leaf LTD  zinatarajiwa kulipwa hivi karibuni na  kampuni hiyo.  

Kwa  mujibu wa taarifa  iliyotolewa kwa vyombo vya  habari RC mrindoko  amesema  anawahakikishia  wakulima   wa Amcos  sita  ambazo  hazijalipwa  Fedha ya mauzo  ya Tumbaku  tayari serikali imefanya jitihada Kupitia   Rais  Dkt  Samia   Saluhu  Hassan amefanya  jitihada kubwa  za kuhakikisha wakulima hao wanalipwa  fedha zao  hivi karibuni  kuanzia tarehe 4 septemba na kuendelea wataanza kulipwa .

Amebainisha kuwa Serikali ya Mkoa wa Katavi  inafahamu  kuna  wakulima  wa Tumbaku  hawajalipwa   fedha zao kwa wakati walizouza  Tumbaku yao  kwa  msimu   wa mauzo ya tumbaku ya  mwaka huu.

Mkurugenzi wa Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya Mkwawa Leaf LTD Ahmed Mansoor Huwel akiwa katika uzinduzi wa Msimu wa Masoko Mapema Mwezi May,2023 Katika Halmashauri ya Nsimbo
 
Amezitaja Amcos  sita  ambazo hazijalipwa fedha zao na  Kampuni ya Mkwawa kuwa ni Nsimbo ,  Bulamata ,Magunga ,Kasekese , Muungano na  Ilunde

Mrindoko  amesema Jumla ya fedha ambazo wakulima wa Amcos  hizo wanazodai Kampuni ya Mkwawa ni Dola  za Kimarekani  Milioni  2.582 tatizo la wakulima kutolipwa fedha zao kwa wakati si  Mkoa wa Katavi peke yake na limetokana na  matatizo ya kiuchumi   duniani  ulisababishwa    na uhaba wa  Dola .

 Hivyo  amewaelekeza  wakuu wa Wilaya wote wa Wilaya zilizopo  katika Mkoa wa Katavi  kusimamia fedha hizo  mara baada ya kuwa  zimeingia kwenye  Akaunti za Amcos    wahakikishe wakulima wanalipwa malipo yao kwa haraka  pasipokuwa na kucheleshwa hata kidogo .

Mrindoko ameeleza kuwa Rais  Dkt  Samia  amefanya kazi kubwa  hivyo  anawahakikishia wakulima wa Mkoa wa Katavi  malipo wanayodai wakulima watalipwa hivi karubuni  kwani wakulima watambue kuwa  Serikali ipo  pamoja nao siku zote   kuhakikisha haki ya kila mkulima inapatikana .

Aidha amewataka wakulima wa zao hilo kuendelea kulima kwa bidi kwani   hawatarajii tena kuona tatizo hilo linaendelea tena kwenye  msimu ujao  wamejipanga  kuondoa  tatizo hilo kwa kuyasimamia kikamilifu makampuni ya ununuzi wa Tumbaku .

Katika  Mkoa wa Katavi  kuna  makampuni  mawili ambayo yanayonunua   Tumbaku  ambayo ni Premium ambayo  imeisha lipo kiasi cha Dola  milioni  19.598 na  wao  hawadaiwi  hata senti  moja na wakulima wao kampuni ya pili ni ya Mkwawa ambao wao wanadaiwa na wakulima kiasi  cha Dola  milioni 2.582.   .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages