MTEPA AACHA SIMAZI KUBWA MPANDA WAKATI MWILI WAKE UKIAGWA.

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapundizi (CCM) Mkoa wa Katavi,Iddy Kimatta akiwa mbele ya jeneza ambalo limehifadhi mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda,Philip Method Mtepa sambamba akiwa ameshika picha yake.

George Mwigulu na Paul Mathias,Mpanda.

MAREHEMU Philip Methond Mtepa,Mwenyekiti  wa Chama Cha Mpindunzi (CCM) Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ameagwa leo katika makazi yake yaliyopo mtaa wa Airtel Manispaa ya Mpanda ambapo leo atasafirishwa kwenda kuzikwa mkoani Rukwa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi,Iddy Kimatta akiwahutubia waombelezaji wa msimba wa aliyekuwa mwenyekiti wa CCM  wilaya ya Mpanda,Philip Method Mtepa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi,Iddy Kimatta amesema kuwa kuna pengo kubwa limeachwa na marehemu kutokana na muda mrefu amekitumikia chama kwa uzalendo mkubwa.

Uzalendo kwa Chama na Taifa wa aliyekuwa mwenyekiti huyo sio wa kutiliwa shaka hata kidogo ambapo vijana wanamambo mengi ya kujifunza kutoka kwake.

Kimatta amasema kuwa Marehemu ni moja ya viongozi ambao walichaguliwa kwenye uchanguzi wa ndani ya chama mwaka 2022 ambapo kwa pamoja walikuwa wamejiwekea malengo makubwa ya kiutendaji yatakayo hakikisha chama kinapiga hatua kubwa ya kuisimamia serikali pamoja ustawi wa chama kiujumla.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko (katikati)akiwa ameketi na waombolezaji wengine ambao wamehudhuria kwenye msiba wa Marehemu Phlip Method Mtepa aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda.

Baadhi ya viongozi wa serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Katavi wakiwa kwenye msimba wa aliyekuuwa mwenyekiti wa CCM Mpanda,Philip Method.


Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Jamila Yusuphu (kulia) akiwa na waombolezaji wengine kawenye msimba wa aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda,Philip Method.
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi,Anna Lupembe (amevaavazi jeupe)pembeni yake kkushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini,Sebastian Kapufi wakiwa na waombolezaji wengine.

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Katavi kwa tiketi ya CCM,Taska Mbogo akiwa na waombolezaji wengine kwenye msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda Philip Method Mtepa.

Beda Katani aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa  wa Katavi akitoa salam za rambirambi kwa waombolezaji.

Wiliam Mbongo,Diwani wa Kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi akiwa ameonesha sura ya huzuni katika msimba wa aliyekuwa mwenyekit wa CCM Wilaya ya Mpanda Philip Mathod Mtepa.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda,Sadiki Kaduro (Kushoto) akiwa na waombolezaji wengine kwenye msiba wa kumuaga aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda Philip Method Mtepa.

Baadhi ya madiwani wa kata mbalimbali za manispaa ya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa na waombolezaji wengine.
Baadhi ya waombolezaji mnalimbali wakiwa kwenye msimba wa kumuaga aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Philip Methiod Mtepa.

Baadhi ya Maofisa wa serikali wakiwa kwenye msiba

Baadhi wananchi wa manispaa ya Mpanda wakizungumza kwa nyakti tofauti,Abdallah Rashidi amesemakuwa wameondokewa na kiongozi muhimu ndani ya chama ambapo watamkumbuka siku zote.

Marehemu Method Mtepa anatalajia kuzikwa 21/9/2023 Katika Kjiji cha Kasanga Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages