RC: KATAVI AIPONGEZA KAMPUNI YA PREMIUM KWA KUWALIPA WAKULIMA WA TUMBAKU

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiongea na wadau wa zao la Tumbaku wakati wa kutiliana saini mikataba ya ununuzi wa Tumbaku na makampuni ya ununuzi wa Tumbaku mkoa wa katavi.


Na Walter Mguluchuma ,Katavi

Mkuu wa mkoa wa Katavi ameipongeza Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya Premium kwa kuwalipa wakulima wa Zao la Tumbaku kwa wakati kwenye vyama vya  Msingi walivyoingia navyo mkataba wa ununuzi wa wa zao la Tumbaku kwa Msimu 2022/2023.


Mkuu wa mkoa wa Katavi ameipongeza Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya Premium kwa kuwalipa wakulima wa Zao la Tumbaku kwa wakati kwenye vyama vya  Msingi walivyoingia navyo mkataba wa ununuzi wa wa zao la Tumbaku kwa Msimu 2022/2023.

Pongezi hizo amezitoa wakati wa Hafla ya Kutiasaini Mikataba ya ununuzi wa Tumbaku na Makampuni ya ununuzi wa zao hilo kwa Msimu ujao wa 2023/2024 Mkuu huyo wa mkoa amesema anawapongeza kampuni ya Premium kwa kuwalipa wakulima kwa muda sahihi hali ambayo imewafanya wakulima hao kuendelea na shuguli zao za kiuchumi.

‘’Nitoe pongezi nyingi sana kwa Kampuni ya Premium ambayo ilikuwa na manunuzi ya fedha zipatazo  Dola Milioni 19 .681 kwa taarifa nilizinazo hapa wameshalipa fedha zao zote ‘’amesema Mrindoko.

Yusuph Mahundi Mwakilishi wa Kampuni ya Premium akisaini mkataba na moja wapo ya chama cha Msingi kwa Msimu ujao wa kilimo wa 2023/2024


Katika hatua nyingine ametoa Siku 12 kwa kampuni ya Mkwawa kuhakikisha inawalipa wakulima wa Tumbaku ambao bado hawalipwa mpaka sasa kiasi cha Dola  Milioni 2.5 kati ya Dola Milioni 6.1 ambapo hadi ssasa zilizoliwpwa ni dola Milioni 3.5.

‘’Nitoe maelekezo kwamba kabla ya September 30 wawe wamewalipa wakulima fedha zao licha kuwa tatizo lao nilakidunia tunaomba deni  hilo  liendelee kupungua ‘’amesema Mrindoko.

Katika hatua nyingine amekemea tabia ya utoroshaji wa Tumbaku ambao kwa baadhi ya maeneo hali mabayo hupelekea kushuka kwa Mapato kwa wakulima na vyama vyao msingi kwa ujumla.

Ameziagiza vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya zote tatu kuendelea kusimamia uzuiaji wa Utoroshwaji wa tumbaku katika mkoa wa Katavi na amewaonya baadhi ya watu wanao jihusisha na ulanguzi wa Tumbaku kwani kufanya hivyo nikinyume na utaratibu na tumbaku itakayo kamatwa itataifishwa yote.

Mrindoko amewaonya tabia ya wakulima kuchukua miti kwaajili ya kupanda na badala yake wamekuwa hawapandi miti hiyo na badala yake kuiweka kwenye nyumba zao na kukauka palepale misitu na uoto wa asili ukiendelea kuharibika kutokana na kuni wanazo kata za kuchomea Tumbaku.

Meneja wa Bodi ya Tumbaku Gerwin Swai amesema pamoja na mkoa wa Katavi kuwa na idadi kubwa ya wakulima wa Tumbaku kuliko maeneo mengine bado uzalishaji wao ni mdogo na hauna Tija.

Swai ameshauri wakulima kulima eneo dogo kwa kuzingatia maelezo ya watalamu na kuziomba mamlaka zinazo sambaza mbolea kwa wakulima kuwafikishia mbolea hizo kwa wakati ili kwenda na majira ya msimu husika.

Peter Nyakunga Mlajisi Msaidizi Mkoa wa Katavi amesema kwa msimu ujao wa kilimo wa mkoa wa katavi umejiwekea lengo la kuzalisha kilo milini 19,028 462  kati ya kilohizo Kampuni ya Premium inakwenda kuingia mkataba wa wa Milioni 14,265 862 na Kampuni ya Mkwa wa Kilo 4,762,600

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages