![]() |
Mwakilishi wa Kampuni ya Ununuzi wa Tumbaku ya Premium Yusuph Mahundi akisaini mkataba wa ununuzi wa Tumbaku na kimoja
wapo cha chama cha msingi cha ushirika ambacho wameingia nacho
mkataba kwa msimu wa 2023/2024
|
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiongea na viongozi wa Vyama vya Ushirika na Makampuni yaliyoingia Mkataba wa ununuzi wa Tumbaku |
Mrajisi msaidizi wa vyama
vya ushirika Mkoa wa Katavi Peter Nyakunga amesema
vyama hivyo vimesaini mikataba na makampuni mawili yanayonunua tumbaku
katika Mkoa wa Katavi ambayo ni Premium na Mkawa kukiwa na lengo
la uzalishaji wa kili 19,028, 462 ambazo zinatarajiwa kuzalishwa katika
msimuujao wa kilimo .
Kktika mikataba
hiyo Kampuni ya Premium imeingia mikataba yenye uzalishaji wa
kilo 14 265 862 na Kampuni ya Mkwawa kili 4,762
600 utiaji huo saini mitakataba umeshudiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Katavi pamoja na viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika
cha Mkoa wa Katavi Latcu wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama,
Bodi ya Tumbaku na wadau mbalimbali wa kilimo .
Nyakunga amebainisha kuwa kanuni namba 36 ya Sheria ya zao la Tumbaku inazungumzia habari za malipo ya wakulima baada ya kuuza tumbaku yao malipo yanatakiwa kufanyika ndani ya siku 14 pamoja na mikataba hiyo iliyosainiwa kwa ibara 25 ibara ya 9.1 inaeleza kuwa mnunuzi na chama kikuu cha ushirika wanahakikisha malipo yanafanyika ndani ya siku 14 baada ya kufanyika kwa soko .
Utaratibu huo wa
kusaini mitakaba ni mpya kwa hapa nchini tofauti na
ulivyokuwa umezoweleka katika misimu yote iliyopita huku lengo kuu
ikiwa ni kuweka uwzi na kuaminiana na utaratibu huo utakwenda
kutatua changamoto zilizikuwa zikijitokeza na kuleta malalamiko .
Meneja wa Bodi ya
Tumbaku Mkoa wa Katavi Genuin Swai amesema zoezi
hilo ni la kihistoria kwani haijawahi kutokea hapa nchini mikataba ya
ununuzi kwenye vyama vya ushirika vya msingi ikashuhudiwa na wadau wote hivyo
ni historia kwa sekta ya tumbaku .
Amesema mikataba hiyo
imefanywa kufatia maelekezo yaliyokuwa yametolewa na waziri wa
Kilimo Hussein Bashe alieagiza mikataba ya msimu huu
ufanyike baina ya makampuni ya ununuzi wa Tumbaku na vyama
walivyonunua tumbaku ya msimu uliopita
Hivyo kila chama
kinatakiwa kuendelea na kampuni yake ya msimu uliopita kwa hali hiyo hata
kama chama kitakataa kuingia mkataba na kampuni yake ya msimu
uliopita kampuni nyingine haiwezi kukichukua ikiwa
ni katika kulinda ushindani ili kuondoa migogoro ya msimu
uliopita na kuongeza mahusiano kati ya hivyo vyama na kampuni na
kuendelea na ushindani wenye tija kuliko kubakia na kampuni moja .
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema Mkoa umeweka utaratibu wa
kusaini mikataba kwa njia ya ili kuondokana na malalamiko.
Ameyataka Makampuni yaliyoingia mkataba na vyama hivyo
kuhakikisha wanawalipa wakulima fedha zao kwa asilimia mia moja kwa mwaka
huu utakuwa wa mwisho hawatakubali kuona kampuni ya ununuzi wa
Tumbaku inashindwa kuwalipa wakulima kwa wakati .
‘’Mkoa hauta vumilia kampuni ambayo inasusua kuwalipa wakulima hivyo agizo hilo walizingatie na walitilie maanani kwani malengo ya Rais na viongozi wa Mkoa wa Katavi ni kuhakikisha wanasimia masilahi ya wakulima ili walipwe malipo yao kwa asilimia mia moja ‘’ amesema Rc Mrindoko
Aidha
katika utiaji saini huo chama cha ushirika cha Msingi cha
Magunga kimekataa kuingia mkataba na Kampuni ya ununuzi
wa Tumbaku ya Mkwawa katika hali ambayo wadau mbalimbali hawakutegemea
kutokea.
Mwenyekiti wa chama
hicho Hamza Makonyi amesema hawako Tayari hawako tayari
kuingia mkataba na Kampuni ya Tumbaku ya Mkwawa kwa kuwa bado
wanawadai malipo ya fedha ya ununuzi wa Tumbaku ya msimu uliopita na uamuzi wa
kuikataa kampuni hiyo ulitolewa na wakulima wa chama hicho
kwenye mkutano mkku uliofanyika tarehe 29/7/2023na barua walisha
mwandikia mkurugenzi wa bodi ya Tumbaku Tanzania .
Meneja wa Bodi ya Tumbaku
Mkoa wa Katavi amekili nakala ya barua hiyo ingawa hadi sasa
hajapokea barua au maelekezo yoyote juu ya majibu ya
barua yao hiyo .