![]() |
Baadhi ya watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Nsimbo wakiwa katika Mafunzo yaliyotolewa na TMDA Kutoka Makao Makuu Dodoma |
Na Jackson Gerald,Mpanda
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba [TMDA]
Makao Mkauu Imetoa mafunzo yakuripoti madhara
namatukio yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba kwawatoa huduma zaAfya.katika
hospitali ya wilaya ya Nsimbo Mkoani katavi ili kuondokana na athari zinazoweza
kutokana namatumizi ya vifaa tiba.
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba [TMDA] Makao Mkauu Imetoa mafunzo yakuripoti madhara namatukio yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba kwawatoa huduma zaAfya.katika hospitali ya wilaya ya Nsimbo Mkoani katavi ili kuondokana na athari zinazoweza kutokana namatumizi ya vifaa tiba.
Akitoa mafunzo kwa watoa huduma
za Afya Afisa usajili dawa kutoka makao
makuu Mamlaka ya dawa na vifaa tiba Dodoma
Davidi Matle amesema kuwa watoa huduma za afya wanapaswa kuripoti Madhara
yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba ili kuondokana na athari zinazo weza
kutokana na matumizi ya vifaa tiba.
Matle amewaomba watoa huduma za Afya kuzingatia elimu hiyo kwa ukubwazaidi ikiwa nipamoja na kuchunguza kubaini nakutoa ripoti zamatukio yatokanayo ma matumizi ya vifaa tiba.Matle ameongeza kuwa si watoa huduma za Afya tu wanao paswa kuzingatia elimu hii bali wanajamii kwa ujumla ili kuweza kubain na kutoa taarifa na hatimae kupata ufumbuzi
‘’Niwaombe watoa huduma za Afya kuweza kubain na kuripoti madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba lakini pia wanajamii kwa ujumla kubain na kutoa taarifa ili kufanya uchunguzi wakina kwa uharaka’’amesema MatleMusa maduka Nimfamasia katika Hospitali ya Wilaya yansimbo amesema kuwa elimu walio ipata kuhusu kuripoti matukio yatokanayo namatumizi ya vifaa tiba itaondoa madhara makubwa yanayoweza kutokana na matumizi ya vifaa tiba Kwawagonjwa ikiwa nipamoja na kudhibiti hatimae kuondoa changamoto ambazo wenda zikazua madhara makubwa zaidi kwa binadamu kutokana na matumizi ya vifaa tiba.
‘’Elimu hii kwakweli imeleta tija sana kwetu sisi kama watoa huduma za Afya kwanza imeturahisishia kujua na kutambua kwa uharaka madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba nahatimae kuripoti kadhia hizo na kwajicho lakiuchunguzi hii itaondoa pengine changamoto ambazo zilikuwa hazijabainika kuweza kuziripoti kwa undani zaidi ili zikaangaliwe kwa jicho la kiuchunguzi’amesema Maduka
Mganga mfawidhi wahospitali hiyo Gregory Mgaya hakusita kuongeza kuwa pamoja na kupewa elimu juu yakuripoti madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba zipo mipango mikakati ambazo wao kama hospitali wataziweka ili kuweza kupata ripoti za kiuchunguzi kuhusu matumizi ya vifaa tiba nakutoa ripoti katika mamlaka husika ilikuongeza nguvu ya utatuzi wa changamoto ambazo wenda zipo na hazijabainika.
‘’Sisi kama hospitali ya Nsimbo
kutokana na elimu hii tulio ipata kutoka[ TMDA] Tuna wahaidi kuwa tunaenda
kuweka mipango mikakati yakuweza kupata taarifa pindi tunapo kuwa tukitumia
vifaa tiba ''anasema Mgaya
Ili kubaini kwa urahisi madhara
ambayo wenda yapo na hayajaripotiwa nakuweza kufanyiwa uchunguzi ili kuondokana
na kadhia hii’’
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba[ TMDA]Inaendelea na mafunzo katika mkoa wakatavi ili kuongeza uelewa kwa watoa huduma za Afya kuweza kuripoti ipasavyo madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba.