Na Walter Mguluchuma,Katavi
Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya amewaonya watu wenye tabia ya kuhalibu miundo mbinu ya barabara kwa kulima kando ya barabara kupitisha wanyama barabarani na wanaoiba alama za barabaran waache tabia hiyo mara moja kwani wanaofanya hivyo watambue kuwa wanaihujumu Serikali
Naibu Waziri wa Ujenzi God frey Kasekenya akitowa maelekezo kwa uongozi wa TANROADS Mkoa wa Katavi kuhakikisha ujenzi wa daraja la mto Kavuu linalounganisha mji mdogo wa Maji Moto naI inyonga ambalo ndio tegemeo kubwa kwa wasafiri wanaosafiri kutoka katika Mikoa ya Songe na Rukwa kwa ajiri ya kwenda Kanda ya Ziwa wahakikishe linakamilika kabla ya mvua kuanza kunyesha ili barabara hiyo isiweze kufungwa na watu kushindwa kusafirisha mazao yao ujenzi wa daraja hilo unagharimu zaidi ya bilioni moja ambapo hapo awali daraja hilo lilikuwa la vyuma
Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya amewaonya watu wenye tabia ya kuhalibu miundo mbinu ya barabara kwa kulima kando ya barabara kupitisha wanyama barabarani na wanaoiba alama za barabaran waache tabia hiyo mara moja kwani wanaofanya hivyo watambue kuwa wanaihujumu Serikali
Agizo hilo amelitoa wakati wa ziara
yake ya siku mbili aliyoifanya Mkoani Katavi ya kukagua maendeleo
Miundo mbinu ya barabara zinazoendelea kutekelezwa kayika
Mkoa wa Katavi inayosimamiwana Wizara ya Ujenzi alipokuwa
akikagua ujenzi wa barabara inayojengwa kwa kiwango cha yenye urefu
wa kilomita 25 kutoka Vikonge Mkoani Katavi kuelekea Uvinza Kigoma .
Kasekenya amebainisha kuwa wapo baadhi ya watu ambao
wamekuwa wakiharibu miundo mbinu ya barabara kwenye maeneo
wanayolima mipunga kwa kufungulia maji kwenye majaruba ya mpinga na
kuyaekekezea barabarani na kupitisha mifugo barabarani
na kusabisha uharibifu wa barabara i .
amesema kumekuwepo pia na uharibifu wa alama za
barabarani na wizi wa alama za barabara jambo ambalo ni
hatari kwa watumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu kwani
kunaweza kusababisha ajari na watu kupoteza maisha .
Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey
Kasekenya akikagua ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 50
kutoka Kibaoni hadi sitalike wakati wa ziara yake Mkoani Katavi ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara zinazoendelea kujengwa Mkoani Katavi
amewataka watu wanye tabia hiyo waache mara moja kwani Serikali imefanya kazi kubwa ya kutengeneza miundo mbinu hiyo na Wizara ya ujenzi haiku tayari kuona uhalibifu huu unaendela kwa kuwa kufanya uhalibifu wa miundo mbinu ni kuhujumu nchi.
Akizungumzia barabara ya Luhafwe kwenda Kigoma
inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami alisema kuwa yatari wameisha
anza kujenga na zipo kilometa 39 kuanzia Mpanda hadi Vikonge zipo
tayari na sasa ni Vikonge hadi Luhafwe lakini
mkandarasi huyo wa Kampuni ya Kichina ya CHICO
ameisha saini mkataba mwingine wa kilometa 37 zitakazofika hadi Mishamo
akiwa anaelekea Kigoma .
amefafanu kuwa zimebaki kilometa
101 barabara hiyo itakuwa imekamilika kabisa hadi Uvinza hata hivyo
Rais Samia Suluhu Hassan ameisha fanya
mazungumzo na Benki ya Afrika za kumalizia hizo kilomeata 101 na mazungumzo
yapo katika hatua za mwisho .
Kesekenya amemusisitiza Mkandarasi na
msimamizi mshauri wa mradi huo kuwa watambue kuwa hiyo
ni barabara kubwa na inapitisha magari mengi makubwa na
mizigo na tukijua kuwa moja ya mikoa inayozalisha mazao mengi ni
Mkoa wa Katavi na hata Kigoma hivyo wakati matengenezo
hayo ya kiwa yanaendelea wahakikishe barabara hiyo inaendelea kupitika
katika kipindi chote cha masika.
amewataka TANROADS Mkoa wa Katavi
kuhakikisha wanamsimamia mkandara huyo kwa karibu ili
barabara ijengwe kama ambavyo ilivyo sanifiwa ili tusitegemee barabara
kuweza kufaei kabla ya muda wake ikitokea hivyo TANROADS watakuwa
wameiangusha Serikali kwa kushirikiana na mkandarasi .
Meneja Msimamizi wa Mradi wa Barabara hiyo
Mhandisi Albert Raizer alisema Ujenzi wa barabara
ya vikonge hadi Luhafwe yenye urefu
wa kilomeata 25 ni utekelezaji wa moja ya ahadi za Rais
Mkoani Katavi kwakuwa barabara hiyo ni kiunganishi kati ya makao makuu
ya Mkoa wa Katavi na Kigoma .
Ujenzi wa barabara hiyo unagharamiwa na fedha za
Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja na itagharimu
kiasi cha shilingi Bilioni 35,638,514,918.00 zikijumlisha na kodi zote na
ushuru isipo kuwa VAT na tarehe awali ya
kumaliza mradi ni 22 Desemba 2023.
Mhandisi Raizer alisema mpaka sasa
hakuna changamoto kubwa kuhusiana na mradi huo ukiondoa
changamoto ya mvua ambayo inafahamika wakati wa kipindi cha masika .
Mkazi wa Kijiji cha Luhafwe John Masanja
ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kutengeneza barabara hiyo
ambayo ni mkombozi kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi na Kigoma na kwa nchi
za Burundi DRC na Rwanda .
Kwa wananchi itasaidia pia kuwapunguzia gharama za
usafiri wanapokuwa wanahitaji kwenda sehemu nyingine kwa kupitia barabara na
alitowa mfano kutoka kwenye kijiji chao hadi makao makuu ya Mkoa
wanatozwa nauli ya Tshs 7000 kwa umbali huo wa kilometa 70.