Na Paul Mathias,Mpanda
Mkuu wa Wikaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema Wilaya ya Mpanda itahakikisha Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Maalumu ya Wasichana inayojegwa Katika Kata ya Kapalala Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi inakamilika kwa wakati ilia ianze kupokea wanafunzi Mnamoa January 2024.
Mkuu wa Wilaya ya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema Wilaya ya Mpanda itahakikisha Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Maalumu ya Wasichana inayojegwa Katika Kata ya Kapalala Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi inakamilika kwa wakati ilia ianze kupokea wanafunzi Mnamo January 2024
Ameyasema hayo wakati
alipotembelea na kujionea Mwenendo wa Ujenzi wa Shule hiyo ya Wasichana Maalumu ambapo
serikali imeleta Shilingi Bilioni Tatu kwaajili ya ujenzi wa Shule
hiyo ya Sekondari ya Wasichana maalumu kwa Wasichana.
‘’tunamshukuru sana Rais Dk Samia
Suluhu Hassan Mradi huu niwakimkoa macho yote ya mkoa yapo hapa kuhakikisha
mradi huu unakamilika kwa wakati na thamani ya Fedha inaonekana Sisi kama
Wilaya ya Mpanda tutahakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati ili ifikapo
January 2024 wanafunzi waanze kutumia Miundombinu hii’’ anasema Jamila
![]() |
Baadhi ya Muonekano wa Majengo ya Madarasa ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maalumu inajengwa katika Kata ya Kapalala Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi. |
‘’tumefika hapa tumetembelea na
kukagua Majengo ya haya kwa macho tumeona Mradi huu unaviwango vinavyotakiwa
nimwagize Mkurugenzi kupitia watalamu wake kuhakikisha mradi huu unaendana na
thamani ya fedha mradi ukamilike kwa wakati ili ifikapo January 2024 Majengo
haya yaanze kutumiwa na wanafunzi’’amesisitiza
Mkuu huyo wa Wilaya.
Katika kuhakikisha upatikanaji wa Maji unakuwa wa Uhakika shuleni hapo Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpanda amewaagiza Ruwasa kuhakikisha wanakamilisha Uchimbaji wa Kisima ili huduma ya Maji iwe ya uhakika baada ya mradi kuanza kutumika.
''Niwaagize Ruwasa kuhakikisha hawa DCCA wanakamilisha kazi ya uchimbaji wa Kisima ambao wameanza kuchimba Halmashauri tayari wameshatoa fedha na tume ona kutokana na maji kutokuwa ya uhakika kuna baadhi ya maeneo mradi upo chini kutokana na ukosefu wa Maji nimtake meneja wa Ruwasa Mkoa kuhakikisha kazi ya kuchimba kisima kwenye eneo hili unakamilika fedha zote walishapewa ''amesema Dc Jamila
Mohamed Ramadhani Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya Nsimbo amesema kuwa watahakisha kuwa mradi huo wa
unakamilika kulingana na muda wa waliopewa na wizara ya Tamisemi ya kuhakisha
ujenzi unakamilika ifikapo 31/12/2023 unakamilika .
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Ramadhani akielezea Maendeleo ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana inayojegwa kwenye Halmashauri hiyo. |
‘’mkakati wetu sasa ni kupata
Madawati pamoja na Vitanda kwaajili ya Mabweni maana bila madawati na Vitanda
kwenye Mabweni hatuwezi kuanza kutumia hii Shule hilo tayari tumeshanza
kulifanyia kazi’’ anasema Mohamed
Katika zaiara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ametemmbelea Shule ya Sekondari Lupembe ambayo ilipatiwa fedha za Serikali kiasi cha Shilingi Milioni 603 kwaajili ya kuongeza miundo mbinu ya Madarasa pamoja na Majengo mengine.