WATU WAWILI WAUAWA KWA KUCHIJWA NA KUTUPWA KANDO YA BARABARA

 

Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Kagwira wakiwa katika mshangao kufuatia watu wawili kuuawa kwa Kuchijwa kwenye Kijiji hicho

Na Paul Mathias,Tanganyika.

Watu wawili wakazi Kitongoji cha Imbambe Kijiji Cha Kagwira Kata ya Kabungu Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wamekutwa wamefariki Dunia kwa Kuchijwa na kutupwa Pembezoni mwa Barabara.

Shira benedictor Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagwira akielezea tukio hilo.

Watu wawili wakazi Kitongoji cha Imbambe Kijiji Cha Kagwira Kata ya Kabungu Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wamekutwa wamefariki Dunia kwa Kuchijwa na kutupwa Pembezoni mwa Barabara.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa Kuamkia leo Kijijini hapo huku wananchi hao wakilaani kitendo hicho cha unyama kilichofanywa na wauaji hao. 

Waliouawa kwa Kuchijwa katika tukio hilo ni Atanas Allyen Miaka 23 mkazi wa Kijiji cha Kabungu pamoja na Katalina Yuna Mkazi wa Kabungu miaka 21.

Wakazi wa Kijiji cha Kagwira wakiwa katika eneo la tukio

Shira Benedictor Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagwira amsema kuwa waliofariki dunia ni wakazi wa Kitongoji cha Ibambe ambao wamefariki dunia kwa kuuawa wakati wa usiku wakitoka Kijiji cha Kabungu ambapo wanafanya shughuli zao.

‘’Nimtu na jirani yake waliouawa  wanaishi kitongoji cha Ibambe tumepata taarifa hii kwa mshtuko sana tunaomba Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi’’ anasema mwenyekiti huyo

Ziada mnayahe afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kabungu amesema kuwa alipata taarifa ya tukio hilo kwa njia ya simu majira ya usiku ambayo alipigiwa na wananchi juu ya tukio hilo la watu kuuawa kwa Kuchijwa.

Ameeleza kuwa baada ya taarifa hizo alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanganyika kwaajili ya uchunguzi zaidi wa Tukio hilo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaster Ngonyani amekili kuwepo kwa tukio hilo na tayari jeshi hilo linawashikilia   watu wawili kwaajili ya mahojiano juu ya Tukio hilo.

Ngonyani ameeleza kuwa tukio hilo linasura ya Wivu wa Kimapenzi kwani wamebaini mmoja ya marehemu alikuwa nawasiliana na watu ambao walikuwa ni wapenzi wake.

‘’katika chanzo chetu tulivyofatilia pale saluni anapafanyia kazi huyu Kijana Atanas walikuwa wanapigiana simu na Mpenzi wake ambae ni Katalina kwamba njoo unapo toka mjini njoo unipitie na kweli akaja akampitia wakaanza safari ya kuelekea Kabungu walipotoka pale ndo kikawakuta kifo’’ anasema Kamanda ngonyani

Katika hatua nyingine amesema jeshi hilo limeanza kufanya upelelezi wa kina juu ya tukio hilo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages